1
1 Pet 3:15-16
Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia
Mwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa hofu. Nanyi mwe na dhamiri njema, ili katika neno lile mnalosingiziwa, watahayarishwe wale wautukanao mwenendo wenu mwema katika Kristo.
Compare
Explore 1 Pet 3:15-16
2
1 Pet 3:12
Kwa kuwa macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, Na masikio yake husikiliza maombi yao; Bali uso wa Bwana ni juu ya watenda mabaya.
Explore 1 Pet 3:12
3
1 Pet 3:3-4
Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi; bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu.
Explore 1 Pet 3:3-4
4
1 Pet 3:10-11
Kwa maana, Atakaye kupenda maisha, Na kuona siku njema, Auzuie ulimi wake usinene mabaya, Na midomo yake isiseme hila. Na aache mabaya, atende mema; Atafute amani, aifuate sana.
Explore 1 Pet 3:10-11
5
1 Pet 3:8-9
Neno la mwisho ni hili; mwe na nia moja, wenye kuhurumiana, wenye kupendana kama ndugu, wasikitikivu, wanyenyekevu; watu wasiolipa baya kwa baya, au laumu kwa laumu; bali wenye kubariki; kwa sababu hayo ndiyo mliyoitiwa ili mrithi baraka.
Explore 1 Pet 3:8-9
6
1 Pet 3:13
Naye ni nani atakayewadhuru, mkiwa wenye juhudi katika mema?
Explore 1 Pet 3:13
7
1 Pet 3:11
Na aache mabaya, atende mema; Atafute amani, aifuate sana.
Explore 1 Pet 3:11
8
1 Pet 3:17
Maana ni afadhali kuteswa kwa kutenda mema, ikiwa ndiyo mapenzi ya Mungu, kuliko kwa kutenda mabaya.
Explore 1 Pet 3:17
Home
Bible
Plans
Videos