Bwana akamwambia Mose: Nenda kwake Farao! Kwani mimi nimeushupaza moyo wake nayo mioyo ya watumishi wake, nipate kuvitoa hivi vielekezo vyangu katikati yao, kusudi wewe uyasimulie masikioni mwa mwanao namo mwa mjukuuu wako, niliyoyafanya huku Misri, navyo vilekezo vyangu, nilivyoviweka kwao, mpate kujua, ya kuwa mimi ni Bwana.