utaniona, nikinyesha kesho saa zizi hizi mvua ya mawe mazito sana, isiyokuwa bado huku Misri yenye nguvu kama hiyo tangu siku ile, misingi yake ilipowekwa, hata sasa. Sasa tuma watu, wayahimize makundi yako nao wote wa kwako walioko mashambani kukimbilia nyumbani! Kwani watu wote, nao nyama wote watakaoonekana mashambani, wasiopelekwa nyumbani watakufa, mvua hiyo ya mawe itakapowanyeshea.