1
Mhubiri 5:2
Biblia Habari Njema
Fikiri kabla ya kusema, wala usiwe mwepesi kusema chochote mbele ya Mungu, kwa maana Mungu yuko mbinguni na wewe uko duniani. Kwa hiyo usiseme mengi.
Compare
Explore Mhubiri 5:2
2
Mhubiri 5:19
Kama Mungu anampa mtu utajiri na mali na kumjalia fursa ya kufurahia hayo, basi binadamu ashukuru na avifaidi hivyo alivyojipatia kwa jasho lake. Hiyo ni zawadi kutoka kwa Mungu.
Explore Mhubiri 5:19
3
Mhubiri 5:10
Apendaye fedha hatatosheka na fedha; wala atamaniye mali hata akiipata hatatosheka. Hilo nalo ni bure kabisa.
Explore Mhubiri 5:10
4
Mhubiri 5:1
Uwe mwangalifu uendapo katika nyumba ya Mungu, na kukaribia ili kusikiliza kwa makini kuliko kutambika kama watambikavyo wapumbavu, watu wasiopambanua kati ya jema na ovu.
Explore Mhubiri 5:1
5
Mhubiri 5:4
Ukimwekea Mungu nadhiri, usikawie kuitimiza; na Mungu hapendezwi na wapumbavu. Tekeleza ulichoahidi.
Explore Mhubiri 5:4
6
Mhubiri 5:5
Ni afadhali kutoweka nadhiri kuliko kuweka nadhiri kisha usiitimize.
Explore Mhubiri 5:5
7
Mhubiri 5:12
Usingizi wa kibarua ni mtamu, awe ameshiba au amekula kidogo tu. Lakini usingizi wa tajiri ni wa wasiwasi daima, maana ziada ya mali yake humsumbua usiku kucha.
Explore Mhubiri 5:12
8
Mhubiri 5:15
Kama vile binadamu alivyokuja duniani uchi toka tumboni mwa mama yake, ndivyo atakavyorudi uchi huko alikotoka. Hataweza kuchukua hata sehemu ndogo ya mapato ya kazi yake.
Explore Mhubiri 5:15
Home
Bible
Plans
Videos