YouVersion Logo
Search Icon

Wagalatia Utangulizi

Utangulizi
Paulo aliandika waraka huu katika safari yake ya kwanza ya kueneza Injili. Baada yake kuondoka Galatia, waumini Wayahudi walifika huko, nao wakaanza kusisitiza kwamba lazima watu wa Mataifa walioamini kwanza watimize Sheria ya Mose ili wapate kuokoka. Paulo aliandika kupinga mafundisho hayo, akionyesha jinsi Abrahamu, ambaye aliishi miaka 400 kabla ya Sheria ya Mose kutolewa, alivyookolewa kwa imani. Alionyesha kwamba kama vile Sheria haingeweza kumwokoa mtu, basi hakuna mtu angeweza kuwa mkamilifu kwa kujitahidi kwa uwezo wake mwenyewe kuitimiza Sheria.
Mwandishi
Mtume Paulo.
Kusudi
Kukataa mafundisho ya kuwa muumini wa Mataifa ni lazima atii sheria za Kiyahudi ndio aokolewe.
Wazo Kuu
Paulo anatetea kwa bidii kweli ya Injili ambayo kiini chake ni kwamba, “Mtu anaokolewa kwa neema ya Mungu kwa kumwamini Kristo.”
Mambo Muhimu
Paulo anasisitiza uhalali wa Injili, ubora wa Injili, na uhuru wa Injili.
Mahali
Antiokia.
Tarehe
Kama 49 B.K.
Wahusika Wakuu
Paulo, Tito, Barnaba, Petro, na walimu wa uongo.
Mgawanyo
Paulo atetea Injili na mamlaka yake kama mtume (1:1–2:21)
Kuwekwa huru kutokana na Sheria (3:1-24)
Ukuu wa Injili juu ya Sheria (3:25–4:31)
Uhuru wa Mkristo (5:1-26)
Mawaidha kuhusu mwenendo wa Mkristo (6:1-18).

Currently Selected:

Wagalatia Utangulizi: NEN

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in