Hesabu 33
33
Vituo Katika Safari Ya Waisraeli
1 Hivi ndivyo vituo katika safari ya Waisraeli walipotoka Misri kwa vikosi chini ya uongozi wa Mose na Aroni. 2 Kwa agizo la Bwana, Mose aliweka kumbukumbu ya vituo katika safari yao. Hivi ndivyo vituo katika safari yao:
3 Waisraeli walisafiri kutoka Ramesesi katika siku ya kumi na tano ya mwezi wa kwanza, siku iliyofuata Pasaka. Walitembea kwa ujasiri wazi mbele ya Wamisri wote, 4 waliokuwa wakizika wazaliwa wao wa kwanza wote, ambao Bwana alikuwa amewaua katikati yao, kwa kuwa Bwana alikuwa ameleta hukumu juu ya miungu yao.
5 Waisraeli waliondoka Ramesesi na kupiga kambi huko Sukothi.
6 Wakaondoka Sukothi na kupiga kambi huko Ethamu, pembeni mwa jangwa.
7 Wakaondoka Ethamu, wakageuka wakarudi Pi-Hahirothi, hadi mashariki ya Baal-Sefoni, wakapiga kambi yao karibu na Migdoli.
8 Wakaondoka Pi-Hahirothi wakapita katikati ya bahari mpaka jangwani, na baada ya kusafiri kwa siku tatu katika Jangwa la Ethamu, walipiga kambi huko Mara.
9 Wakaondoka Mara wakaenda Elimu, mahali ambapo palikuwa na chemchemi kumi na mbili na mitende sabini, huko wakapiga kambi.
10 Wakaondoka Elimu na kupiga kambi kando ya Bahari ya Shamu.
11 Wakaondoka kando ya Bahari ya Shamu na kupiga kambi katika Jangwa la Sini.
12Wakaondoka katika Jangwa la Sini, wakapiga kambi huko Dofka.
13Wakaondoka Dofka, wakapiga kambi huko Alushi.
14 Wakaondoka Alushi, wakapiga kambi Refidimu, mahali ambapo hapakuwa na maji kwa ajili ya watu kunywa.
15 Wakaondoka Refidimu na kupiga kambi katika Jangwa la Sinai.
16 Wakaondoka katika Jangwa la Sinai na kupiga kambi huko Kibroth-Hataava.
17 Wakaondoka Kibroth-Hataava na kupiga kambi huko Haserothi.
18 Wakaondoka Haserothi na kupiga kambi huko Rithma.
19Wakaondoka Rithma na kupiga kambi huko Rimon-Peresi.
20 Wakaondoka Rimon-Peresi na kupiga kambi huko Libna.
21Wakaondoka Libna na kupiga kambi huko Risa.
22Wakaondoka Risa na kupiga kambi huko Kehelatha.
23Wakaondoka Kehelatha na kupiga kambi kwenye mlima Sheferi.
24Wakaondoka kwenye mlima Sheferi na kupiga kambi huko Harada.
25Wakaondoka Harada na kupiga kambi huko Makelothi.
26Wakaondoka Makelothi na kupiga kambi huko Tahathi.
27Wakaondoka Tahathi na kupiga kambi huko Tera.
28Wakaondoka Tera na kupiga kambi huko Mithka.
29Wakaondoka Mithka na kupiga kambi huko Hashmona.
30 Wakaondoka Hashmona na kupiga kambi Moserothi.
31 Wakaondoka Moserothi na kupiga kambi huko Bene-Yakani.
32 Wakaondoka Bene-Yakani na kupiga kambi huko Hor-Hagidgadi.
33 Wakaondoka Hor-Hagidgadi na kupiga kambi huko Yotbatha.
34Wakaondoka Yotbatha na kupiga kambi huko Abrona.
35 Wakaondoka Abrona na kupiga kambi huko Esion-Geberi.
36 Wakaondoka Esion-Geberi na kupiga kambi huko Kadeshi katika Jangwa la Sini.
37 Wakaondoka Kadeshi na kupiga kambi kwenye Mlima Hori, mpakani mwa Edomu. 38 Kwa amri ya Bwana, kuhani Aroni alipanda Mlima Hori, mahali alipofia katika siku ya kwanza ya mwezi wa tano, mwaka wa arobaini baada ya Waisraeli kutoka Misri. 39Aroni alikufa juu ya Mlima Hori akiwa na umri wa miaka 123.
40 Mfalme Mkanaani wa Aradi, ambaye aliishi huko Negebu ya Kanaani, akasikia kwamba Waisraeli wanakuja.
41Wakaondoka kwenye mlima Hori na kupiga kambi huko Salmona.
42Wakaondoka Salmona, wakapiga kambi huko Punoni.
43 Wakaondoka Punoni, wakapiga kambi huko Obothi.
44 Wakaondoka Obothi, wakapiga kambi huko Iye-Abarimu, mipakani mwa Moabu.
45 Wakaondoka Iye-Abarimu, wakapiga kambi huko Dibon-Gadi.
46 Wakaondoka Dibon-Gadi na kupiga kambi huko Almon-Diblathaimu.
47 Wakaondoka Almon-Diblathaimu na kupiga kambi katika milima ya Abarimu, karibu na Nebo.
48 Wakaondoka kwenye milima ya Abarimu na kupiga kambi kwenye tambarare ya Moabu, kando ya Yordani ngʼambo ya Yeriko. 49 Huko kwenye tambarare za Moabu walipiga kambi kandokando ya Mto Yordani, kuanzia Beth-Yeshimothi mpaka Abel-Shitimu.
50 Katika tambarare za Moabu kando ya Yordani kuvukia Yeriko, Bwana akamwambia Mose, 51 “Sema na Waisraeli uwaambie: ‘Mtakapovuka Mto Yordani kuingia Kanaani, 52 wafukuzeni wakazi wote wa nchi iliyo mbele yenu. Haribuni sanamu zao zote za kuchongwa, na sanamu zilizotengenezwa kwa kuyeyusha chuma, na kupabomoa mahali pao pa ibada. 53 Mtaimiliki nchi hiyo na kukaa huko, kwa kuwa nimewapeni ninyi kuimiliki. 54 Mtaigawanya nchi hiyo kwa kupiga kura, kufuatana na koo zenu. Kwa kundi kubwa zaidi toa urithi mkubwa zaidi, na kwa kundi dogo zaidi urithi mdogo zaidi. Chochote kinachowaangukia kwa kura kitakuwa chao. Mtaigawanya nchi kufuatana na makabila ya babu zenu.
55 “ ‘Lakini kama hamkuwafukuza wenyeji wakaao katika nchi hiyo, wale mtakaowaruhusu wabaki watakuwa kama sindano kwenye macho yenu na miiba kwenu kila upande. Watawasumbua katika nchi mtakayoishi. 56 Kisha nitawatenda ninyi kile ambacho nimepanga kuwatenda wao.’ ”
Currently Selected:
Hesabu 33: NEN
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Neno: Biblia Takatifu™ Neno™
Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015 na Biblica, Inc.
Imetumiwa kwa ruhusa. Haki zote zimehifadhiwa duniani kote.
Kiswahili Contemporary Version™
Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.
Used with Permission. All Rights Reserved Worldwide.