YouVersion Logo
Search Icon

Filemoni 1

1
Salamu
1Paulo, mfungwa wa Al-Masihi Isa, pamoja na Timotheo ndugu yetu.
Kwa Filemoni rafiki yetu mpendwa na mtendakazi mwenzetu, 2kwa dada yetu mpendwa Afia, kwa Arkipo askari mwenzetu na kwa kundi la waumini wanaokutana nyumbani mwako.
3Neema na amani zitokazo kwa Mungu, Baba#1:3 Kwa mwanadamu, Mwenyezi Mungu ni Baba kupitia uhusiano unaopatikana katika kumtumaini Isa Al-Masihi. yetu, na kwa Bwana wetu Isa Al-Masihi ziwe nanyi.
Shukrani na maombi
4Siku zote ninamshukuru Mungu wangu ninapokukumbuka katika maombi yangu, 5kwa sababu ninasikia kuhusu imani yako katika Bwana Isa na upendo wako kwa watakatifu wote. 6Naomba utiwe nguvu katika kushiriki imani yako na wengine, ili upate kuwa na ufahamu mkamilifu wa kila kitu chema tunachoshiriki kwa ajili ya Al-Masihi. 7Upendo wako umenifurahisha mno na kunitia moyo, kwa sababu wewe ndugu, umeiburudisha mioyo ya watakatifu.
Paulo anamtetea Onesimo
8Hata hivyo, ingawa katika Al-Masihi ningekuwa na ujasiri wa kukuagiza yale yakupasayo kutenda, 9lakini ninakuomba kwa upendo. Mimi Paulo, mzee na pia sasa nikiwa mfungwa wa Al-Masihi Isa, 10nakuomba kwa ajili ya mwanangu Onesimo#1:10 maana yake Wa manufaa, aliyefanyika mwanangu nilipokuwa kwenye minyororo. 11Mwanzoni alikuwa hakufai, lakini sasa anakufaa sana wewe na mimi pia.
12Namtuma kwako, yeye aliye moyo wangu hasa. 13Ningependa nikae naye ili ashike nafasi yako ya kunisaidia wakati huu nikiwa kifungoni kwa ajili ya Injili. 14Lakini sikutaka kufanya lolote bila idhini yako, ili wema wowote uufanyao usiwe wa lazima, bali wa hiari. 15Huenda sababu ya Onesimo kutengwa nawe kwa muda ni ili uwe naye daima, 16si kama mtumwa sasa, bali bora kuliko mtumwa, kama ndugu mpendwa. Yeye ni mpendwa sana kwangu na hata kwako zaidi, yeye kama mwanadamu na kama ndugu katika Bwana Isa.
17Hivyo kama unanihesabu mimi kuwa mshirika nawe, mkaribishe kama vile ungenikaribisha mimi mwenyewe. 18Kama amekukosea lolote au kama unamdai chochote, nidai mimi. 19Ni mimi Paulo, ninayeandika waraka huu kwa mkono wangu mwenyewe. Nitakulipa hilo deni. Kumbuka kwamba nakudai hata nafsi yako. 20Ndugu yangu, natamani nipate faida kwako katika Bwana Isa, yaani uniburudishe moyo wangu katika Al-Masihi. 21Huku nikiwa na hakika ya kutii kwako, nakuandikia nikijua kwamba utafanya hata zaidi ya yale ninayokuomba.
22Jambo moja zaidi: Niandalie chumba cha wageni, kwa kuwa nataraji kurudishwa kwenu kama jibu la maombi yenu.
Salamu za mwisho
23Epafra, aliye mfungwa mwenzangu katika Al-Masihi Isa, anakusalimu.
24Vivyo hivyo Marko, Aristarko, Dema na Luka, watendakazi wenzangu wanakusalimu.
25Neema ya Bwana Isa Al-Masihi iwe pamoja na roho zenu. Amen.

Currently Selected:

Filemoni 1: NENO

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in