Zaburi 119:1-11
Zaburi 119:1-11 NENO
Heri wale walio waadilifu katika njia zao, wanaoenenda katika Torati ya Mwenyezi Mungu. Heri wale wanaozishika shuhuda zake, wanaomtafuta kwa moyo wao wote. Wasiofanya lolote lililo baya, wanaoenenda katika njia zake. Umetoa maagizo yako ili tuyatii kwa ukamilifu. Laiti mwenendo wangu ungekuwa imara katika kuyatii maagizo yako! Hivyo mimi sitaaibishwa ninapozingatia amri zako zote. Nitakusifu kwa moyo mnyofu ninapojifunza sheria zako za haki. Nitayatii maagizo yako; usiniache kabisa. Kijana aisafishe njia yake jinsi gani? Ni kwa kutii, akilifuata neno lako. Ninakutafuta kwa moyo wangu wote, usiniache niende mbali na amri zako. Nimelificha neno lako moyoni mwangu ili nisikutende dhambi.