YouVersion Logo
Search Icon

Zaburi 91:1-9

Zaburi 91:1-9 NENO

Yeye akaaye mahali pa salama pake Yeye Aliye Juu Sana, atadumu katika uvuli wake Mwenyezi. Nitasema kumhusu Mwenyezi Mungu, “Yeye ndiye kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu, ninayemtumaini.” Hakika yeye ataniokoa na mtego wa mwindaji, na maradhi ya kuambukiza ya kuua. Atakufunika kwa manyoya yake, chini ya mabawa yake utapata kimbilio, uaminifu wake utakuwa ngao na kinga yako. Hutaogopa vitisho vya usiku, wala mshale urukao mchana, wala maradhi ya kuambukiza yanayonyemelea gizani, wala tauni iharibuyo adhuhuri. Ijapo watu elfu wataangukia kando yako, kumi elfu mkono wako wa kuume, lakini haitakukaribia wewe. Utatazama tu kwa macho yako na kuona adhabu ya waovu. Ukimfanya Aliye Juu Sana kuwa makao yako; naam, Mwenyezi Mungu ambaye ni kimbilio langu