YouVersion Logo
Search Icon

Zaburi 93

93
Zaburi 93
Mwenyezi Mungu ni mkuu
1Mwenyezi Mungu anatawala, amejivika utukufu;
Mwenyezi Mungu amejivika utukufu
tena amejivika nguvu.
Dunia imewekwa imara,
haitaondoshwa.
2Kiti chako cha enzi kimekuwa thabiti tangu zamani;
wewe umekuwa tangu milele.
3Bahari zimepaza, Ee Mwenyezi Mungu,
bahari zimepaza sauti zake;
bahari zimepaza sauti za mawimbi yake.
4Yeye ni mkuu kuliko ngurumo ya maji makuu,
ni mkuu kuliko mawimbi ya bahari:
Mwenyezi Mungu aishiye juu sana ni mkuu.
5Ee Mwenyezi Mungu, sheria zako ni imara;
utakatifu umepamba nyumba yako
pasipo mwisho.

Currently Selected:

Zaburi 93: NENO

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in