1 Tim 5
5
Huduma kwa Waumini
1 #
Law 19:32
Mzee usimkemee, bali umwonye kama baba; na vijana kama ndugu; 2wanawake wazee kama mama; wanawake vijana kama ndugu wa kike; katika usafi wote. 3Uwaheshimu wajane walio wajane kweli kweli. 4Lakini mjane akiwa ana watoto au wajukuu, na wajifunze kwanza kuyatenda yaliyo wajibu wao kwa jamaa zao wenyewe, na kuwalipa wazazi wao. Kwa kuwa hili lakubalika mbele za Mungu. 5#Yer 49:11; Lk 2:37; 18:7Basi yeye aliye mjane kweli kweli, ameachwa peke yake, huyo amemwekea Mungu tumaini lake, naye hudumu katika maombi na sala mchana na usiku. 6Bali, yeye asiyejizuia nafsi yake amekufa ingawa yu hai. 7Mambo hayo pia uyaagize, ili wasiwe na lawama. 8Lakini mtu ye yote asiyewatunza walio wake, yaani, wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini. 9Mjane asiandikwe isipokuwa umri wake amepata miaka sitini; naye amekuwa mke wa mume mmoja; 10#Ebr 13:2; Yn 13:14naye ameshuhudiwa kwa matendo mema; ikiwa amelea watoto, ikiwa amekaribisha wageni, ikiwa amewaosha watakatifu miguu, ikiwa amewasaidia wateswao, ikiwa amefuata kwa bidii kila tendo jema. 11Bali wajane walio vijana ukatae kuwaandika hao, maana, wakizidiwa na tamaa kinyume cha Kristo, wataka kuolewa; 12nao wana hukumu kwa kuwa wameiacha imani yao ya kwanza. 13#2 The 3:11Tena, pamoja na hayo, hujifunza kuwa wavivu, wakizunguka-zunguka nyumba kwa nyumba; wala si wavivu tu, lakini ni wachongezi na wadadisi, wakinena maneno yasiyowapasa. 14#1 Kor 7:9Basi napenda wajane, ambao si wazee, waolewe, wazae watoto, wawe na madaraka ya nyumbani; ili wasimpe adui nafasi ya kulaumu. 15Kwa maana wengine wamekwisha kugeuka na kumfuata Shetani. 16Mwanamke aaminiye, akiwa ana wajane, na awasaidie mwenyewe, Kanisa lisilemewe; ili liwasaidie wale walio wajane kweli kweli.
17 #
Rum 12:8; Flp 2:29 Wazee watawalao vema na wahesabiwe kustahili heshima maradufu; hasa wao wajitaabishao kwa kuhutubu na kufundisha. 18#Kum 25:4; 24:15; 1 Kor 9:9; Mt 10:10; Lk 10:7Kwa maana andiko lasema, Usimfunge kinywa ng’ombe apurapo nafaka. Na tena, Mtenda kazi astahili ujira wake. 19#Kum 17:6; 19:15; Mt 18:16; 2 Kor 13:1Usikubali mashitaka juu ya mzee, ila kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu. 20#Gal 2:14Wale wadumuo kutenda dhambi uwakemee mbele ya wote, ili na wengine waogope. 21#Lk 9:26Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Kristo Yesu, na mbele za malaika wateule, uyatende hayo pasipo kuhukumu kwa haraka; usifanye neno lo lote kwa upendeleo. 22#1 Tim 4:14Usimwekee mtu mikono kwa haraka, wala usizishiriki dhambi za watu wengine. Ujilinde nafsi yako uwe safi. 23Tokea sasa usinywe maji tu lakini tumia mvinyo kidogo, kwa ajili ya tumbo lako, na magonjwa yakupatayo mara kwa mara.
24Dhambi za watu wengine zi dhahiri, zatangulia kwenda hukumuni; wengine dhambi zao zawafuata. 25Vivyo hivyo matendo yaliyo mazuri ya dhahiri; wala yale yasiyo dhahiri hayawezi kusitirika.
Currently Selected:
1 Tim 5: SUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.