YouVersion Logo
Search Icon

2 Nya 11

11
Yuda na Benyamini Wajiimarisha
1 # 1 Fal 12:21 Hata Rehoboamu alipofika Yerusalemu, akakusanya nyumba ya Yuda na Benyamini, watu wateule mia na themanini elfu waliokuwa hodari, watu wa vita, ili wapigane juu ya Israeli, ili wamrudishie Rehoboamu huo ufalme. 2#Kum 33:1; 1 Sam 2:27; 1 Fal 12:22-24; 2 Nya 8:14; 12:15; 1 Tim 6:11Lakini neno la BWANA likamjia Shemaya mtu wa Mungu, kusema, 3Mwambie Rehoboamu mwana wa Sulemani, mfalme wa Yuda, uwaambie na Israeli wote waliomo Yuda na Benyamini, ukisema, 4BWANA asema hivi, Hamtapanda wala kupigana na ndugu zenu; rudini kila mtu nyumbani kwake; kwa kuwa jambo hili limetoka kwangu. Basi, wakayasikiliza maneno ya BWANA, wakarudi katika kumwendea Yeroboamu.
5Naye Rehoboamu akakaa Yerusalemu, akajenga miji yenye ngome katika Yuda. 6#Mwa 35:19; 1 Sam 17:12; Mt 2:1; Amu 15:8; 1 Nya 4:31; 2 Sam 14:2; 2 Nya 20:20; Neh 3:5; Yer 6:1; Amo 1:1Akajenga na Bethlehemu, na Etamu, na Tekoa, 7na Bethsuri, na Soko, na Adulamu, 8na Gathi, na Maresha, na Zifu, 9na Adoraimu, na Lakishi, na Azeka, 10na Sora, na Aiyaloni, na Hebroni, iliyoko katika Yuda na Benyamini, miji yenye maboma. 11Akazifanya imara hizo ngome, akaweka majemadari humo, na akiba ya vyakula, na mafuta, na mvinyo. 12Na ndani ya miji yote mmoja mmoja aliweka ngao na mikuki, akaifanya kuwa na nguvu nyingi mno. Yuda na Benyamini ikawa milki yake.
Makuhani na Walawi Wamuunga Rehoboamu Mkono
13Wakamwendea makuhani na Walawi waliokuwa katika Israeli yote, kutoka mpaka wao wote. 14#Hes 35:2; Yos 21:20-42; 1 Fal 12:28-33; 2 Nya 13:9Kwani Walawi wakaacha malisho yao, na milki yao, wakaja Yuda na Yerusalemu; kwa sababu Yeroboamu na wanawe waliwatupa, ili wasimfanyie BWANA ukuhani; 15#1 Fal 12:31; 13:33; 14:9; Hos 13:2; Law 17:7; Kum 32:15-17; 1 Kor 10:20; Ufu 16:14; 1 Fal 12:28naye akajiwekea makuhani wa mahali pa juu, na wa wale majini, na wa zile ndama alizozifanya. 16#2 Nya 15:9; 30:11; Zab 69:32Na kutoka katika kabila zote za Israeli, wakaandamwa na hao waliojikaza nia kumtafuta BWANA, Mungu wa Israeli, wakaja Yerusalemu, ili wamtolee dhabihu BWANA, Mungu wa baba zao. 17#2 Nya 12:1; Hos 6:4; Mt 13:18Hivyo wakaufanya imara kwa miaka mitatu ufalme wa Yuda, na kumtia nguvu Rehoboamu mwana wa Sulemani; kwa maana muda wa miaka mitatu wakaiendea njia ya Daudi na Sulemani.
Ndoa za Rehoboamu
18Rehoboamu akaoa mke, Mahalathi binti Yerimothi mwana wa Daudi, na wa Abihaili binti Eliabu, mwana wa Yese; 19#1 Fal 15:2akamzalia wana, Yeushi, na Shemaria, na Zahamu. 20Kisha baada yake akamwoa Maaka, binti Absalomu; na yeye akamzalia Abiya, na Atai, na Ziza, na Shelomithi. 21Rehoboamu akampenda Maaka binti Absalomu kuliko wakeze wote na masuria yake; (maana alioa wake kumi na wanane, na masuria sitini, akazaa wana ishirini na wanane na binti sitini). 22#Kum 21:15-17Rehoboamu akamsimamisha Abiya, mwana wa Maaka, kuwa mkuu, mtawala kati ya nduguze, kwa kuwa aliazimia kumtawaza awe mfalme. 23#Kum 17:17; 1 Fal 11:3Akafanya kwa akili, akawatawanya wanawe wote kati ya nchi zote za Yuda na Benyamini, katika kila mji wenye boma; akawapa vyakula tele. Akawatafutia wake wengi.

Currently Selected:

2 Nya 11: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in