YouVersion Logo
Search Icon

2 Nya 33

33
Kutawala kwa Manase
1 # 2 Fal 21:1 Manase alikuwa na umri wa miaka kumi na miwili alipoanza kutawala; akatawala katika Yerusalemu miaka hamsini na mitano. 2#Law 18:24-30; Kum 18:9; 2 Fal 17:11,15; 2 Nya 28:3Akafanya yaliyo maovu machoni pa BWANA, sawasawa na machukizo yote ya mataifa, aliowafukuza BWANA mbele ya wana wa Israeli. 3#2 Fal 18:4; 2 Nya 30:14; 31:1; Kum 16:21; 4:19; 17:3; 2 Fal 23:5-11; Yer 8:2; Sef 1:5Kwa maana akapajenga tena mahali pa juu alipopabomoa Hezekia babaye; akazisimamisha madhabahu za mabaali, akafanya na sanamu za maashera, akaabudu jeshi lote la mbinguni, na kulitumikia. 4#Kum 12:11; 1 Fal 8:29Akajenga madhabahu katika nyumba ya BWANA, napo ndipo alipopanena BWANA, Katika Yerusalemu litakuwako jina langu milele. 5#2 Nya 4:9Akajenga madhabahu kwa ajili ya jeshi lote la mbinguni katika nyua mbili za nyumba ya BWANA. 6#Law 18:21; Kum 18:10; 2 Nya 28:3; Eze 23:37; 2 Fal 21:6Tena akawapitisha wanawe motoni katika bonde la mwana wa Hinomu; akatazama bao, akabashiri, akafanya uganga, akajishughulisha na hao wenye pepo wa utambuzi, na wachawi; akafanya mabaya mengi machoni pa BWANA, hata kumkasirisha. 7#2 Fal 21:7; Zab 132:14Akaiweka sanamu ya kuchonga aliyoifanya, katika nyumba ya Mungu ambayo Mungu alimwambia Daudi, na Sulemani mwanawe, Katika nyumba hii, na katika Yerusalemu, niliouchagua miongoni mwa kabila zote za Israeli, nitaliweka jina langu milele; 8#2 Sam 7:10wala sitawaondoshea miguu tena Israeli katika nchi niliyowaagizia baba zenu; wakiangalia tu kutenda yote niliyowaamuru, yaani, torati yote, na sheria, na maagizo, niliyowaamuru kwa mkono wa Musa.
Manase Atubu na Kujirudi
9Basi Manase akawakosesha Yuda na wenyeji wa Yerusalemu, hata wakazidi kufanya mabaya kuliko mataifa, aliowaharibu BWANA mbele ya wana wa Israeli. 10#Neh 9:29; Yer 25:4Naye BWANA akasema na Manase, na watu wake; wala wasiangalie. 11#Kum 28:36; Ayu 36:8; Zab 107:10,11Kwa hiyo BWANA akaleta juu yao maakida wa jeshi la mfalme wa Ashuru, waliomkamata Manase kwa minyororo, wakamfunga kwa pingu, wakamchukua mpaka Babeli. 12#Kum 4:30,31; Zab 118:5; 120:1; Yer 31:18-20; Hos 5:15; Yon 2:2; Mik 6:9; Lk 15:16-18; Kut 10:3; 2 Nya 32:26; Lk 18:4; 1 Pet 5:6Hata alipokuwa katika taabu, akamsihi BWANA, Mungu wake, akajinyenyekeza sana mbele za Mungu wa baba zake. 13#1 Nya 5:20; Ezr 8:23; Zab 142:1-7; Omb 3:55,56; Zab 9:16; Dan 4:25Akamwomba; naye akamtakabali, akayasikia maombi yake; akamrudisha tena Yerusalemu katika ufalme wake. Ndipo Manase akajua ya kwamba BWANA ndiye Mungu.
14 # 1 Fal 1:33; 2 Nya 27:3 Hata baada ya hayo akaujengea mji wa Daudi ukuta wa nje, upande wa magharibi wa Gihoni, bondeni, hata kufika maingilio ya lango la samaki; akauzungusha Ofeli, akauinua juu sana; akaweka maakida mashujaa katika miji yote ya Yuda yenye maboma. 15Akaiondoa miungu migeni, na hiyo sanamu nyumbani mwa BWANA, na madhabahu zote alizozijenga katika mlima wa nyumba ya BWANA, na Yerusalemu, akazitupa nje ya mji. 16#Law 7:12Akaijenga madhabahu ya BWANA, akatoa juu yake dhabihu za sadaka za amani, na za shukrani, akawaamuru Yuda wamtumikie BWANA, Mungu wa Israeli. 17#1 Fal 22:43; 2 Fal 15:4; 2 Nya 15:17; 32:12Lakini watu wakaendelea kutoa dhabihu katika mahali pa juu, ila wakamtolea BWANA, Mungu wao tu.
Kufa kwa Manase
18Basi mambo yote ya Manase yaliyosalia, na maombi yake kwa Mungu wake, na maneno ya waonaji walionena naye kwa jina la BWANA, Mungu wa Israeli, tazama, yameandikwa kati ya mambo ya wafalme wa Israeli. 19Sala yake pia, na jinsi Mungu alivyomtakabali, na dhambi yake yote, na kosa lake, na mahali alipopajenga mahali pa juu, na kupasimamishia maashera na sanamu za kuchonga, kabla ya kujinyenyekeza; tazama, hayo yameandikwa katika tarehe ya Hozai. 20Basi Manase akalala na babaze, wakamzika nyumbani mwake; na Amoni mwanawe akatawala mahali pake.
Kutawala kwa Amoni na Kifo chake
21Amoni alikuwa na umri wa miaka ishirini na miwili alipoanza kutawala; akatawala katika Yerusalemu miaka miwili. 22Akafanya yaliyo maovu machoni pa BWANA, kama alivyofanya Manase babaye; Amoni akazitolea dhabihu sanamu zote alizozifanya Manase babaye, akazitumikia. 23#2 Tim 3:13Wala hakujinyenyekeza mbele za BWANA, kama Manase babaye alivyojinyenyekeza; lakini huyo Amoni akaongeza makosa juu ya makosa. 24#2 Fal 21:23,24; 2 Nya 24:25,26; 25:27,28; Zab 55:23Wakamfanyia fitina watumishi wake, wakamwua katika nyumba yake mwenyewe. 25Lakini watu wa nchi wakawaua wote waliomfanyia fitina mfalme Amoni; watu wa nchi wakamfanya Yosia mwanawe awe mfalme badala yake.

Currently Selected:

2 Nya 33: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in