YouVersion Logo
Search Icon

2 Fal UTANGULIZI

UTANGULIZI
Sehemu ya pili iitwayo Kitabu cha Pili cha Wafalme ni maendelezo ya simulizi la pale Kitabu cha Kwanza kilipoishia (tazama maelezo katika Utangulizi wa Kitabu cha Kwanza cha Wafalme). Sehemu hii inaanza kwa habari za Mfalme Ahazia wa Israeli na maisha ya manabii Eliya na Elisha. Kutokana na uasi na ukaidi wa wafalme wa Israeli, Mungu aliruhusu mfalme wa Ashuru kuivamia Samaria na watu wengi kupelekwa uhamishoni.
Majanga yaliyowapata wakazi wa Israeli baadaye yaliwapata wakazi wa Yuda pia. Mfalme wa Babeli alivamia Yerusalemu akauharibu, akachukua viongozi na watu mashuhuri akawapeleka Babeli.
Maafa yaliyokumba falme hizi mbili yalitokana na uasi wao kwa BWANA. Kila utawala ulipimwa kwa mizani ya uaminifu wake kwa BWANA sio mafanikio yake katika maendeleo, utengamano, uchumi na siasa tu. Ndiposa kuanguka kwa Israeli kunahesabiwa kuwa ni hukumu ya BWANA dhidi ya uasi huo (17:7-23; 25:1-21). Hata hivyo tumaini la wokovu kwamba Mungu atawahurumia na kutimiza Agano lake kwa nyumba ya Daudi liliendelea kuwapo.
Yaliyomo:
1. Mwisho wa Maisha ya Ahazia na Eliya, Sura 1:1–2:12
2. Nabii Elisha, Sura 2:13–8:15
3. Wafalme wa Yuda na Israeli na kuangamizwa kwa Samaria, Sura 8:16–17:41
4. Nyakati za Hezekia na Yosia, Sura 18:1–23:30
5. Wafalme wa mwisho wa Yuda, Sura 23:31–24:20
6. Kuangamizwa kwa Yerusalemu, Sura 25

Currently Selected:

2 Fal UTANGULIZI: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in