YouVersion Logo
Search Icon

Kol 1

1
Salamu
1 # Efe 1:1 Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, na Timotheo, ndugu yetu, 2#Rum 1:7; Efe 1:2kwa ndugu watakatifu, waaminifu katika Kristo, walioko Kolosai. Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu.
Paulo Amshukuru Mungu kwa ajili ya Wakolosai
3 # 1 Kor 13:13; Efe 1:16; 1 The 1:2,3 Twamshukuru Mungu, Baba yake Bwana wetu Yesu Kristo, siku zote tukiwaombea; 4#Efe 1:15tangu tuliposikia habari za imani yenu katika Kristo Yesu, na upendo mlio nao kwa watakatifu wote; 5#1 Pet 1:4; Efe 1:13,18kwa sababu ya tumaini mlilowekewa akiba mbinguni; ambalo habari zake mlizisikia zamani kwa neno la kweli ya Injili; 6#1 Tim 3:16; Efe 1:13iliyofika kwenu, kama ilivyo katika ulimwengu wote, na kuzaa matunda na kukua, kama inavyokua kwenu pia, tangu siku mlipoisikia mkaifahamu sana neema ya Mungu katika kweli; 7#Kol 4:12; Flm 1:23kama mlivyofundishwa na Epafra, mjoli wetu mpenzi, aliye mhudumu mwaminifu wa Kristo kwa ajili yenu; 8naye alitueleza upendo wenu katika Roho.
9 # Efe 1:8,9,15-17; Flp 1:9 Kwa sababu hiyo sisi nasi, tangu siku ile tuliposikia, hatuachi kufanya maombi na dua kwa ajili yenu, ili mjazwe maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote na ufahamu wa rohoni; 10#Efe 1:17; 2:10; 4:1; Flp 1:27mwenende kama ulivyo wajibu wenu kwa Bwana, mkimpendeza kabisa; mkizaa matunda kwa kila kazi njema, na kuzidi katika maarifa ya Mungu; 11#1 Kor 1:5; Efe 1:18,19; 3:16mkiwezeshwa kwa uwezo wote, kwa kadiri ya nguvu ya utukufu wake, mpate kuwa na saburi ya kila namna na uvumilivu pamoja na furaha; 12#Efe 1:11,18mkimshukuru Baba, aliyewastahilisha kupokea sehemu ya urithi wa watakatifu katika nuru. 13#Kol 2:15; Lk 22:53; Efe 2:2; 6:12; 1:6Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake; 14#Efe 1:7ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi;
Ukuu wa Kristo
15 # Ebr 1:3; 2 Kor 4:4; 1 Tim 6:16; Yn 1:18 naye ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote. 16#Yn 1:3,10; Efe 1:10,21Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake. 17#Mit 8:25-27; Efe 1:22Naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika yeye. 18#Efe 1:22-23; 4:15; 5:23; Mdo 4:2; 26:23; Ufu 1:5Naye ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha kanisa; naye ni mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu, ili kwamba awe mtangulizi katika yote. 19#Efe 1:23; Kol 2:9; Yn 1:16Kwa kuwa katika yeye ilipendeza utimilifu wote ukae; 20#Efe 1:7,10; 2:13,16; 1 Yoh 2:2na kwa yeye kuvipatanisha vitu vyote na nafsi yake akiisha kufanya amani kwa damu ya msalaba wake; kwa yeye, ikiwa ni vitu vilivyo juu ya nchi, au vilivyo mbinguni. 21#Efe 2:1,12; 4:18; Rum 5:10Na ninyi, mliokuwa hapo kwanza mmefarikishwa, tena adui katika nia zenu, kwa matendo yenu mabaya, amewapatanisha sasa; 22#Efe 2:11,14,16; 5:27katika mwili wa nyama yake, kwa kufa kwake, ili awalete ninyi mbele zake, watakatifu, wasio na mawaa wala lawama; 23#Mk 16:15; 1 Tim 3:16; Efe 3:17; Ebr 3:14mkidumu tu katika ile imani, hali mmewekwa juu ya msingi, mkawa imara; msipogeuzwa na kuliacha tumaini la Injili mliyosikia habari zake, iliyohubiriwa katika viumbe vyote vilivyo chini ya mbingu; ambayo mimi Paulo nalikuwa mhudumu wake.
Nia ya Paulo kwa Wakolosai
24 # Efe 3:1,13 Sasa nayafurahia mateso niliyo nayo kwa ajili yenu; tena nayatimiliza katika mwili wangu yale yaliyopungua ya mateso ya Kristo, kwa ajili ya mwili wake, yaani, kanisa lake; 25#Efe 3:2,7,8ambalo nimefanywa mhudumu wake, sawasawa na uwakili wa Mungu, niliopewa kwa faida yenu, nilitimize neno la Mungu; 26#Rum 16:25,26; Efe 3:3,5,9,10siri ile iliyofichwa tangu zamani zote na tangu vizazi vyote, bali sasa imefunuliwa kwa watakatifu wake; 27#1 Tim 1:1; Rum 16:25; Efe 3:9; 1:18ambao Mungu alipenda kuwajulisha jinsi ulivyo utajiri wa utukufu wa siri hii katika Mataifa, nao ni Kristo ndani yenu, tumaini la utukufu 28#Efe 4:13ambaye sisi tunamhubiri habari zake tukimwonya kila mtu, na kumfundisha kila mtu katika hekima yote, tupate kumleta kila mtu mtimilifu katika Kristo. 29#Flp 4:13; Efe 3:7,20Nami najitaabisha kwa neno lilo hilo, nikijitahidi kwa kadiri ya kutenda kazi kwake atendaye kazi ndani yangu kwa nguvu.

Currently Selected:

Kol 1: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in