YouVersion Logo
Search Icon

Kum 1

1
Kumbukumbu ya Yaliyotokea Horebu
1 # Hes 32:6,20,29; Yos 9:1; 22:4,7 Haya ndiyo maneno Musa aliyowaambia Israeli wote ng’ambo ya Yordani barani, katika Araba lililoelekea Sufu, kati ya Parani, na Tofeli, na Labani, na Hazerothi, na Dizahabu. 2#Hes 13:26; Kum 9:23Ni mwendo wa siku kumi na moja kutoka Horebu kwa njia ya mlima wa Seiri mpaka Kadesh-barnea. 3#Hes 33:38Ikawa mwaka wa arobaini, mwezi wa kumi na moja, siku ya kwanza ya mwezi, Musa akawaambia wana wa Israeli kama yote aliyopewa na BWANA ya kuwaamuru; 4#Hes 21:21-35; Neh 9:22; Zab 135:11; 139:19alipokwisha kumpiga Sihoni mfalme wa Waamori, aliyekuwa akikaa Heshboni, na Ogu mfalme wa Bashani, aliyekuwa akikaa Ashtarothi iliyo katika Edrei; 5ni ng’ambo ya Yordani katika nchi ya Moabu, alipoanza Musa kufunua torati hii, akisema, 6#Kut 3:11; 9:1; Hes 10:11BWANA, Mungu wetu, alituambia huko Horebu, akasema, Mlivyokaa katika mlima huu vyatosha; 7geukeni mshike safari yenu mwende nchi ya milima ya Waamori, na mahali pote palipo karibu ya hapo, katika hiyo Araba, na nchi ya vilima-vilima, na huko Shefela, na Negebu, na pwani-pwani, nchi ya Wakanaani, na Lebanoni, mpaka mto huo mkubwa, mto wa Frati. 8#Mwa 12:7; 15:18; 28:13Angalieni, nimewawekea nchi mbele yenu, ingieni mkaimiliki nchi BWANA aliyowaapia baba zenu, Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, kwamba atawapa na uzao wao baada yao.
Viongozi wa Makabila Wateuliwa
9 # Kut 18:18; Hes 11:14 Nami wakati ule niliwaambia, nikasema, Siwezi mimi mwenyewe kuwachukua peke yangu. 10#Mwa 15:5; 22:17; 28:14; Kut 32:13; Kum 10:22; 28:62; 1 Nya 27:23BWANA, Mungu wenu, amewafanya kuwa wengi, nanyi, angalieni, mmekuwa leo mfano wa nyota za mbinguni kwa wingi. 11#Mwa 22:17; 26:4; Kut 32:13BWANA, Mungu wa baba zenu, na awafanye kuwa wengi mara elfu kuliko mlivyo, na kuwabarikia, kama alivyowaahidi. 12#1 Fal 3:8; 2 Kor 11:28Nitachukuaje peke yangu mimi mwenyewe udhia wenu, na mzigo wenu, na mateto yenu? 13Jitwalieni watu wenye akili na fahamu, watu wanaojulikana, kwa kadiri ya kabila zenu, nami nitawafanya wawe vichwa juu yenu. 14Nanyi mkanijibu, mkaniambia, Jambo ulilonena ni jema la kufanya. 15Basi nikatwaa vichwa vya kabila zenu wenye akili, waliojulikana, nikawafanya wawe vichwa juu yenu, maakida ya elfu elfu, na maakida ya mia mia, na maakida ya hamsini hamsini, na maakida ya kumi kumi, na wenye amri, kwa kadiri ya kabila zenu. 16#Kut 23:2-8; Yn 7:24; Law 24:22Nikawaagiza wakati ule waamuzi wenu, nikawaambia, Sikizeni ninyi maneno kati ya ndugu zenu, mkaamue kwa haki kati ya mtu na nduguye, na mgeni aliye pamoja naye. 17#1 Sam 16:7; Mit 24:23; Yak 2:1; Mit 28:21; 29:4,25; 2 Nya 19:6; Kut 18:22,26Msitazame nafsi za watu katika hukumu; mwasikize wadogo na wakubwa sawasawa; msiche uso wa mtu awaye yote; kwa kuwa hukumu ni ya Mungu; na lile neno liwashindalo mniletee mimi, nami nitalisikiza. 18Nikawaamuru wakati huo mambo yote yaliyowapasa ninyi kuyafanya.
Waisraeli Wakataa Kuingia katika Nchi
19 # Hes 10:12; Kum 8:15; Yer 2:6; Hes 13:26 Tukasafiri kutoka Horebu, tukapita katikati ya jangwa lile kubwa la kutisha mliloliona, njia ile ya kuiendea nchi ya vilima vya Waamori, kama BWANA, Mungu wetu, alivyotuamuru, tukafika Kadesh-barnea. 20Nami nikawaambia, Mmefika nchi ya vilima ya Waamori, anayotupa sisi BWANA, Mungu wetu. 21#Hes 13:30; 14:8,9; Yos 1:9; Zab 27:1-3; 46:1,7,11; Isa 41:10; 43:1,2; Lk 12:32; Ebr 13:6Tazama, BWANA, Mungu wako, ameiweka nchi mbele yako; haya panda, itamalaki, kama BWANA, Mungu wa baba zako, alivyokuambia; usiogope wala usifadhaike. 22Nanyi mkanikaribia kila mmoja wenu, mkasema, Na tupeleke watu mbele yetu, ili watupelelezee nchi na kutuletea habari za njia itupasayo kuipandia, na za miji tutakayoifikia. 23#Hes 13:3Neno hili likanipendeza sana; nikatwaa watu kumi na wawili, mtu mmoja wa kila kabila. 24Nao wakageuka, wakapanda mlimani wakafika bonde la Eshkoli, wakalipeleleza. 25Wakatwaa baadhi ya matunda ya nchi ile mikononi mwao, wakatuletea huku chini, wakatuletea habari tena, wakasema, Nchi hii anayotupa BWANA, Mungu wetu, ni nchi njema.
26 # Kum 9:23; Ebr 3:16; Hes 14:1-4; Zab 106:24 Lakini hamkukubali kukwea huko, mlihalifu neno la BWANA, Mungu wenu; 27#Kum 9:28mkanung’unika hemani mwenu, mkasema, Ni kwa sababu BWANA ametuchukia, ndipo akatutoa katika nchi ya Misri, apate kututia katika mikono ya Waamori, ili kutuangamiza. 28#Hes 13:28-33; Kum 9:1,2Twakwea kwenda wapi? Ndugu zetu wameiyeyusha mioyo yetu, wakituambia, Wale watu ni wengi, ni warefu kuliko sisi; miji nayo ni mikubwa, imejengewa kuta hata mbinguni; na zaidi ya hayo huko tumewaona Waanaki. 29Ndipo nikawaambieni, Msifanye hofu, wala msiwache. 30#Kut 14:14; Neh 4:20BWANA, Mungu wenu, anayetangulia mbele yenu, ndiye atakayewapigania, kwa mfano wa yote aliyowafanyia huko Misri mbele ya macho yenu; 31#Mdo 13:18; Kut 19:4; Kum 32:11; Isa 46:3,4; 63:9; Hos 11:3na huko jangwani, ulipoona alivyokuchukua BWANA, Mungu wako, kama mtu amchukuavyo mwanawe, njia yote mliyoiendea, hata mkafikilia mahali hapa.
32 # Ebr 3:19; Zab 106:24; Yud 1:5 Lakini katika jambo hili hamkumwamini BWANA, Mungu wenu, 33#Kut 13:21; Zab 78:14; Hes 10:33; Eze 20:6aliyewatangulia njiani, usiku kwa moto, kuwaonyesha njia mtakayoiendea, na mchana kwa hilo wingu, ili apate kuwatafutia mahali pa kusimamisha hema zenu.
Adhabu kwa ajili ya Uasi wa Israeli
34 # Ebr 3:18; Kum 2:14 BWANA akaisikia sauti ya maneno yenu, akaghadhibika, akaapa, akasema, 35#Hes 14:22; Zab 95:11Hakika yangu hapana mmoja miongoni mwa watu hawa wa kizazi hiki kibaya atakayeiona nchi hiyo nzuri, niliyowaapia baba zenu kuwapa, 36isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune, huyo ataiona; nami nitampa yeye na watoto wake nchi hiyo aliyoikanyaga; kwa kuwa amemfuata BWANA kwa kila neno. 37#Hes 27:14; Kum 3:26; 4:21; 34:4; Zab 106:32Na BWANA alinikasirikia mimi kwa ajili yenu, akasema, Wala wewe hutaingia humo; 38#Kut 24:13; 33:11; 1 Sam 16:22; Kum 31:7,23Yoshua mwana wa Nuni asimamaye mbele yako ndiye atakayeingia; mtie moyo; kwa kuwa yeye atawarithisha Israeli. 39#Isa 7:15,16; Eze 18:20Tena, wadogo wenu, mliosema watakuwa mateka, na wana wenu, wasiokuwa leo na maarifa ya mabaya wala mema, ndio watakaoingia, nao ndio nitakaowapa, nao wataimiliki. 40Na ninyi basi geukeni, mshike safari yenu, mwende jangwani kwa njia ya Bahari ya Shamu. 41Ndipo mkanijibu, mkaniambia, Sisi tumefanya dhambi juu ya BWANA, tutakwea kupigana kwa mfano wa yote tuliyoamriwa na BWANA. Mkajifunga kila mtu silaha zake za vita, mkafanya wepesi kukwea mlimani. 42BWANA akaniambia, Uwaambie, Msiende, wala msipigane; kwani mimi si kati yenu; msije mkapigwa mbele ya adui zenu. 43#Hes 14:44,45Basi niliwaambia, msinisikize, bali mliasi amri ya BWANA, mkajikinai, na kukwea mlimani. 44#Kum 28:25; 32:30; Zab 118:12; Isa 7:18Na Waamori waliokuwa wakikaa katika mlima huo, waliwatokea juu yenu, wakawafukuza, kama wafukuzwao na nyuki, wakawapomoshea Seiri mpaka Horma. 45#Ayu 27:9; Zab 66:18; Mit 1:24; Isa 1:15; Yer 11:7-14; Zek 7:11; Yn 9:31Mkarudi mkalia mbele za BWANA; BWANA asiisikize sauti yenu, wala hakuelekeza masikio yake kwenu.
Maisha ya Jangwani
46 # Hes 13:25; 20:1,22; Amu 11:17 Ndipo mkakaa Kadeshi siku nyingi, kwa kadiri ya hizo siku mlizokaa.

Currently Selected:

Kum 1: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in