YouVersion Logo
Search Icon

Ezr UTANGULIZI

UTANGULIZI
Ezra anayefikiriwa kuwa mwandishi wa Kitabu hiki alikuwa kuhani, mwandishi wa Mfalme Artashasta na mmoja wa viongozi wa Wayahudi waliporudi kutoka uhamishoni (7:11-12). Maana ya jina Ezra ni “msaada”. Ezra alitumia maandiko kadhaa ili kukamilisha kitabu hiki (1:2-4; 2:1-70; 4:7-22; 5:6-17; 6:3-12).
Mwandishi anaanza kwa habari za tangazo rasmi la Mfalme Koreshi wa Persia, linaloruhusu Wayahudi kurejea makwao na kujenga upya Hekalu la Yerusalemu (1:1-11). Wayahudi wengi walirudi Yuda wakaanza kujenga madhabahu na kufanya ibada kwa BWANA (2:1-70; 3:1-6), vile vile kuanzisha ujenzi wa Hekalu. Kazi hii ilikumbana na upinzani mkubwa hata hivyo waliweza kumaliza ujenzi wa Hekalu na kuta zake (3:7-6:22).
Mfalme Artashasta wa Persia alimtuma kuhani Ezra kufufua, kusimamia na kurekebisha maisha ya kidini katika Yerusalemu. Naye Ezra alitekeleza agizo hilo. Kimsingi kitabu hiki kinaonyesha maisha ya kidini na kijamii mjini Yerusalemu. Aidha mafaniko yalitokana na juhudi za makusudi katika kuitii sheria ya Mungu. Pale sheria ilipokuwa imevunjwa toba na marejeo vilifanywa na ilipokuwa imepuuzwa utii ulilazimishwa.
Yaliyomo:
1. Wayahudi kurudi toka uhamishoni, Sura 1–2
2. Ujenzi wa Hekalu katika Yerusalemu, Sura 3–6
3. Kurudi kwake Ezra na matengenezo ya jumuiya, Sura 7–10

Currently Selected:

Ezr UTANGULIZI: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in