Mwa 29
29
Yakobo Akutana na Raheli
1 #
Hes 23:7; Hos 12:12 Kisha Yakobo akashika njia yake, akafika nchi ya wana wa mashariki.
2Naye akaangalia, na tazama, kiko kisima kondeni, na makundi matatu ya kondoo yamelala karibu nacho, kwa sababu katika kisima kile hunywesha makundi; na palikuwa na jiwe kubwa juu ya kinywa cha kisima. 3Makundi yote hukusanyika huko, watu wakafingirisha hilo jiwe katika kinywa cha kisima wakawanywesha kondoo, na kulirudisha jiwe juu ya kinywa cha kisima mahali pake. 4Yakobo akawauliza, Ndugu zangu, watu wa wapi ninyi? Wakasema, Tu wa Harani sisi. 5Akawauliza, Je! Mnamjua Labani, mwana wa Nahori? Wakasema, Tunamjua. 6#Mwa 43:27Akawauliza, Je! Hajambo? Wakasema, Hajambo; tazama, Raheli binti yake anakuja na kondoo. 7Akasema, Tazama, ukali mchana bado, wala sio wakati wa kukusanya wanyama; wanywesheni kondoo, mwende kuwalisha. 8Wakasema, Hatuwezi, hata yakusanyike makundi yote, watu wakafingirishe jiwe katika kinywa cha kisima, ndipo tunapowanywesha kondoo.
9 #
Kut 2:16
Hata alipokuwa akisema nao, Raheli akaja na kondoo za baba yake, maana aliwachunga. 10#Kut 2:17Ikawa Yakobo alipomwona Raheli binti Labani, ndugu wa mamaye, na kondoo za Labani, ndugu wa mamaye, Yakobo akakaribia, na kulifingirisha lile jiwe litoke katika kinywa cha kisima, akawanywesha kondoo za Labani, ndugu wa mamaye.
11 #
Mwa 33:4; 45:14; Rum 16:16; 1 Kor 16:20; 2 Kor 13:12; 1 Pet 5:14 Yakobo akambusu Raheli, akainua sauti yake akalia. 12#Mwa 13:8; 24:28Yakobo akamwarifu Raheli ya kuwa yeye ni ndugu wa babaye, na ya kuwa ni mwana wa Rebeka. Basi akapiga mbio akampasha babaye habari. 13#Mwa 24:29Ikawa Labani aliposikia habari za Yakobo, mwana wa nduguye, akaenda mbio amlaki, akamkumbatia, akambusu, akamleta nyumbani kwake. Naye akamwambia Labani maneno hayo yote. 14#Mwa 2:23; Amu 9:2; 2 Sam 5:1; 19:12,13Labani akamwambia, Ndiwe kweli mfupa wangu na nyama yangu. Naye akakaa kwake muda wa mwezi mmoja.
Yakobo Awaoa Mabinti wa Labani
15Labani akamwambia Yakobo, Kwa sababu wewe ni ndugu yangu, basi, je! Unitumikie bure? Niambie mshahara wako utakuwa nini? 16Labani alikuwa na binti wawili, jina la mkubwa ni Lea, na jina la mdogo ni Raheli. 17Naye Lea macho yake yalikuwa dhaifu, lakini Raheli alikuwa mzuri wa umbo, na mzuri uso. 18#Mwa 31:41; 2 Sam 3:14Yakobo akampenda Raheli akasema, Nitakutumikia miaka saba kwa kumpata Raheli, binti yako mdogo. 19Labani akasema, Afadhali nikupe wewe kuliko mtu mwingine; kaa kwangu. 20#Mwa 30:26; Wim 8:7Yakobo akatumika miaka saba kwa kumpata Raheli. Ikawa machoni pake kama siku chache tu kwa vile alivyompenda. 21#Amu 15:1Yakobo akamwambia Labani, Nipe mke wangu, maana siku zangu zimetimia; niingie kwake. 22#Amu 14:10; Yn 2:1Labani akakusanya watu wote wa mahali pale, akafanya karamu. 23Ikawa wakati wa jioni akamtwaa Lea, binti yake, akamletea Yakobo, naye akaingia kwake. 24Labani akampa Lea mjakazi wake Zilpa, awe mjakazi wake. 25Ikawa, kulipokuwa asubuhi, kumbe! Ni Lea. Akamwambia Labani, Nini hii uliyonitenda? 26Sikukutumikia kwa Raheli? Mbona umenidanganya? Labani akasema, Havitendeki hivi kwetu, kumtoa mdogo kabla ya mkubwa; 27#Amu 14:12timiza siku zake saba, nasi tutakupa huyu naye kwa utumishi utakaonitumikia, miaka saba mingine.
28Yakobo akafanya hivi, akatimiza siku zake saba. Naye akampa Raheli binti yake kuwa mkewe. 29Labani akampa binti yake Raheli mjakazi wake Bilha, awe mjakazi wake. 30#Mwa 30:26; 31:41; Hos 12:12Akaingia kwa Raheli naye, akampenda Raheli kuliko Lea, akatumika kwa ajili yake miaka saba mingine.
31 #
Zab 127:3; Mwa 30:1 BWANA akaona ya kwamba Lea hakupendwa, naye akafungua tumbo lake; bali Raheli alikuwa hazai. 32#Kut 3:7; 4:31; Kum 26:7; Zab 25:18; 106:44Lea akapata mimba akazaa mwana, akampa jina lake, Reubeni, maana alisema, Kwa kuwa BWANA ameona teso langu; sasa mume wangu atanipenda. 33Akapata mimba tena akazaa mwana, akasema, Kwa kuwa BWANA amesikia ya kwamba mimi sikupendwa, amenipa na huyu; akamwita jina lake Simeoni. 34Akapata mimba tena, akazaa mwana, akasema, Basi wakati huu mume wangu ataungana nami, kwa sababu nimemzalia wana watatu. Kwa hiyo akamwita jina lake Lawi. 35Akapata mimba tena, akazaa mwana. Akasema, Mara hii nitamsifu BWANA; kwa hiyo akamwita jina lake Yuda; akaacha kuzaa.
Currently Selected:
Mwa 29: SUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.