YouVersion Logo
Search Icon

Ebr 4

4
Pumziko Aliloahidi Mungu
1 # Zab 95:11 Basi, ikiwa ikaliko ahadi ya kuingia katika raha yake, na tuogope, mmoja wenu asije akaonekana ameikosa. 2Maana ni kweli, sisi nasi tumehubiriwa habari njema vile vile kama hao. Lakini neno lile lililosikiwa halikuwafaa hao, kwa sababu halikuchanganyika na imani ndani yao waliosikia. 3#Zab 95:11Maana sisi tulioamini tunaingia katika raha ile; kama vile alivyosema,
Kama nilivyoapa kwa hasira yangu,
Hawataingia rahani mwangu:
ijapokuwa zile kazi zilimalizika tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu. 4#Mwa 2:2Kwa maana ameinena siku ya saba mahali fulani hivi, Mungu alistarehe siku ya saba, akaziacha kazi zake zote; 5#Zab 95:11na hapa napo, Hawataingia rahani mwangu. 6Basi, kwa kuwa neno hili limebaki kwamba wako watu watakaoingia humo, na wale waliohubiriwa habari ile zamani walikosa kuingia kwa sababu ya kuasi kwao, 7#Zab 95:7-8aweka tena siku fulani, akisema katika Daudi baada ya muda mwingi namna hii, Leo; kama ilivyonenwa tangu zamani,
Leo, kama mtaisikia sauti yake,
Msifanye migumu mioyo yenu.
8 # Kum 31:7; Yos 22:4 Maana kama Yoshua angaliwapa raha, asingaliinena siku nyingine baadaye. 9Basi, imesalia raha ya sabato kwa watu wa Mungu. 10#Mwa 2:2; Ufu 14:13Kwa maana yeye aliyeingia katika raha yake amestarehe mwenyewe katika kazi yake, kama vile Mungu alivyostarehe katika kazi zake. 11Basi, na tufanye bidii kuingia katika raha ile, ili kwamba mtu ye yote asije akaanguka kwa mfano uo huo wa kuasi. 12#Yer 23:29; Isa 49:2; Efe 6:17; Yn 12:48; Ufu 19:15Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo. 13Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu.
Yesu Aliye Kuhani Mkuu
14 # Ebr 3:1; 6:20; 7:26; 8:1; 9:11 Basi, iwapo tunaye kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, na tuyashike sana maungamo yetu. 15#Ebr 2:17Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi. 16#1 Yoh 3:21; Rum 3:25Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.

Currently Selected:

Ebr 4: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in