Hos 6
6
Mwito wa Toba
1 #
Ayu 5:18; Kut 15:26; Isa 30:26; Yer 30:17; Eze 34:16 Njoni, tumrudie BWANA; maana yeye amerarua, na yeye atatuponya; yeye amepiga, na yeye atatufunga jeraha zetu. 2Baada ya siku mbili atatufufua; siku ya tatu atatuinua, nasi tutaishi mbele zake. 3#Mit 2:1-9; Mt 13:11; Ayu 29:23Nasi na tujue, naam, tukaendelee kumjua BWANA; kutokea kwake ni yakini kama asubuhi; naye atatujilia kama mvua, kama mvua ya vuli iinyweshayo nchi.
Uovu wa Israeli na Yuda
4Ee Efraimu, nikutendee nini? Ee Yuda, nikutendee nini? Kwa maana fadhili zenu ni kama wingu la asubuhi na kama umande utowekao mapema. 5#Yer 1:10; Ebr 4:12Kwa sababu hiyo nimewakata-kata kwa vinywa vya manabii; nimewaua kwa maneno ya kinywa changu; na hukumu yangu itatokea kama mwanga. 6#Mit 21:3; Zab 50:8; Yn 17:3; Mt 9:13; 12:7Maana nataka fadhili wala si sadaka; na kumjua Mungu kuliko sadaka za kuteketezwa. 7Lakini wao wamelivunja hilo agano kama Adamu; huko wamenitenda mambo ya hiana. 8Gileadi ni mji wa hao watendao maovu, umetiwa rangi ya damu. 9Na kama vile makundi ya wanyang’anyi wamwoteavyo mtu, ndivyo kundi la makuhani wauavyo katika njia ielekeayo Shekemu; naam, wametenda mambo maovu sana. 10Katika nyumba ya Israeli nimeona jambo bovu kabisa; huko uzinzi umeonekana katika Efraimu; Israeli ametiwa unajisi. 11#Zab 126:1Tena, Ee Yuda, wewe umeandikiwa mavuno, hapo nitakapowarudisha wafungwa wa watu wangu.
Currently Selected:
Hos 6: SUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.