YouVersion Logo
Search Icon

Isa 17

17
Utabiri juu ya Dameski
1 # 2 Fal 16:9; Yer 49:23-27; Amo 1:3-5; Zek 9:1 Ufunuo juu ya Dameski. Tazama, Dameski umeondolewa usiwe mji, nao utakuwa chungu ya magofu. 2#Yer 7:33Miji ya Aroeri imeachwa; itakuwa kwa makundi ya kondoo, nao watajilaza huko wala hapana atakayewatia hofu. 3#Isa 7:16Na ngome ya Efraimu itakomeshwa, na ufalme wa Dameski, na mabaki ya Shamu; watakuwa kama utukufu wa wana wa Israeli, asema BWANA wa majeshi.
4 # Isa 10:16 Tena itakuwa katika siku hiyo, utukufu wa Yakobo utapungua-pungua, na kunona kwa mwili wake kutakonda. 5#Yer 51:33; Ufu 14:15-19Tena itakuwa kama hapo avunaye ashikapo mabua ya ngano, na mkono wake ukatapo masuke; tena itakuwa kama hapo mtu aokotapo masuke katika bonde la Warefai. 6Lakini kilichosazwa na mvunaji kitakuwa ndani yake, kama vile wakati wa kupiga mizeituni, matunda mawili matatu yaliyo juu sana; matunda manne matano katika matawi, matawi ya mti wa matunda, asema BWANA, Mungu wa Israeli. 7#2 Nya 30:11; Zab 34:5; Hos 5:15; Mik 7:7; Zek 12:10Katika siku hiyo mwanadamu atamwangalia Muumba wake, na macho yake yatamtazama Mtakatifu wa Israeli. 8Wala hataziangalia madhabahu, kazi ya mikono yake; wala hatavitazama vilivyofanyika kwa vidole vyake, maashera na sanamu za jua. 9Katika siku hiyo miji yake yenye maboma itakuwa kama mahali palipoachwa ndani ya mwitu, na juu ya kilele cha mlima, palipoachwa mbele ya wana wa Israeli; napo patakuwa ganjo. 10#Zab 106:13,21Maana umemsahau Mungu wa wokovu wako, wala hukuukumbuka mwamba wa ngome yako; kwa sababu hiyo ulipanda mashamba yapendezayo, na kutia ndani yake mizabibu migeni. 11Katika siku ile ulipopanda, ulifanya kitalu, na wakati wa asubuhi ulizimeesha mbegu zako, lakini mavuno yatatoweka siku ya huzuni, na ya sikitiko la moyo lifishalo.
12Aha! Uvumi wa watu wengi!
Wanavuma kama uvumi wa bahari;
Aha! Ngurumo ya mataifa!
Wananguruma kama ngurumo ya maji mengi;
13Mataifa wananguruma kama ngurumo ya maji mengi;
Lakini atawakemea, nao watakimbia mbali sana,
Watafukuzwa kama makapi milimani mbele ya upepo,
Na kama mavumbi vuruvuru mbele ya tufani.
14 # Amu 5:31; Mit 22:23; Zab 8:3,9 Wakati wa jioni, tazama, kuna hofu;
Na kabla ya mapambazuko hawako;
Hilo ndilo fungu lao watutekao,
Na ajali yao wanaotunyang’anya mali zetu.

Currently Selected:

Isa 17: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in