YouVersion Logo
Search Icon

Yak 4

4
Urafiki na Ulimwengu
1 # Rum 7:23; 1 Pet 2:11 Vita vyatoka wapi, na mapigano yaliyoko kati yenu yatoka wapi? Si humu, katika tamaa zenu zifanyazo vita katika viungo vyenu? 2Mwatamani, wala hamna kitu, mwaua na kuona wivu, wala hamwezi kupata. Mwafanya vita na kupigana, wala hamna kitu kwa kuwa hamwombi! 3Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu. 4#Lk 6:26; Rum 8:7; 1 Yoh 2:15Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu. 5#Kut 20:3,5; Mt 6:24; Gal 5:17Au mwadhani ya kwamba maandiko yasema bure? Huyo Roho akaaye ndani yetu hututamani kiasi cha kuona wivu? 6#Mit 3:34; Ayu 22:29; Mt 23:12; 1 Pet 5:5Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu. 7#Efe 6:12; 1 Pet 5:8,9Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia. 8#Zek 1:3; Isa 1:16Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili. 9Huzunikeni na kuomboleza na kulia. Kucheka kwenu na kugeuzwe kuwa kuomboleza, na furaha yenu kuwa hamu. 10#1 Pet 5:6Jidhilini mbele za Bwana, naye atawakuza.
Onyo dhidi ya Kumhukumu Mwingine
11Ndugu, msisingiziane; amsingiziaye ndugu yake, au kumhukumu ndugu yake, huisingizia sheria na kuihukumu sheria. Lakini ukiihukumu sheria, huwi mtenda sheria, bali umekuwa hakimu. 12#Mk 7:1; Rum 2:1; 14:4Mtoa sheria na mwenye kuhukumu ni mmoja tu, ndiye awezaye kuokoa na kuangamiza. U nani wewe umhukumuye mtu mwingine?
Kujivuna juu ya Kesho
13 # Mit 27:1 Haya basi, ninyi msemao, Leo au kesho tutaingia katika mji fulani na kukaa humo mwaka mzima, na kufanya biashara na kupata faida; 14#Lk 12:20; Zab 39:5,11walakini hamjui yatakayokuwako kesho. Uzima wenu ni nini? Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa kitambo, kisha hutoweka. 15#Mdo 18:21Badala ya kusema, Bwana akipenda, tutakuwa hai na kufanya hivi au hivi. 16Lakini sasa mwajisifu katika majivuno yenu; kujisifu kote kwa namna hii ni kubaya. 17#Lk 12:47; Rum 14:23Basi yeye ajuaye kutenda mema, wala hayatendi, kwake huyo ni dhambi.

Currently Selected:

Yak 4: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

Videos for Yak 4