YouVersion Logo
Search Icon

Yer 24

24
Tini Zuri na Baya
1 # Amo 7:1; 2 Fal 24:12; 2 Nya 36:10; Yer 22:24 BWANA akanionyesha, na tazama, vikapu viwili vya tini, vimewekwa mbele ya hekalu la BWANA, baada ya Nebukadreza, mfalme wa Babeli, kumchukua mateka Yekonia, mwana wa Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, na wakuu wa Yuda, pamoja na mafundi na wafua chuma, kutoka Yerusalemu, kuwaleta Babeli. 2Kikapu kimoja kilikuwa na tini nzuri sana, kama tini zilizotangulia kuiva; na kikapu cha pili kilikuwa na tini mbovu sana zisizoweza kuliwa, kwa kuwa zilikuwa mbovu sana. 3Ndipo BWANA akaniambia, Unaona nini Yeremia? Nikasema, Naona tini; tini nzuri zilizo nzuri sana; na tini mbovu zilizo mbovu sana, zisizoweza kuliwa, kwa kuwa ni mbovu sana. 4Kisha neno la BWANA likanijia, kusema, 5#Zek 13:9; Ebr 2:11BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Kama zilivyo tini hizi nzuri, ndivyo nitakavyowaangalia mateka wa Yuda, niliowatoa katika mahali hapa, waende mpaka nchi ya Wakaldayo, wapate mema. 6#Eze 36:24; Yer 12:15; 23:3; 32:41; 33:7Kwa maana nitawatulizia macho yangu, wapate mema, nami nitawaingiza katika nchi hii tena; nami nitawajenga, wala sitawabomoa; nitawapanda wala sitawang’oa. 7#Kum 30:6; Isa 51:16; Eze 11:19; 14:11; Yer 7:23; 30:22; 29:13; Zek 8:8; Zab 119:2Nami nitawapa moyo, wanijue ya kuwa mimi ni BWANA; nao watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao; kwa maana watanirudia kwa moyo wao wote. 8#Yer 29:17; 43:1Na habari za tini zile mbovu, zisizoweza kuliwa, kwa kuwa ni mbovu sana; hakika, asema, BWANA, ndivyo nitakavyomtoa Sedekia, mfalme wa Yuda, na wakuu wake, na mabaki ya Yerusalemu, waliosalia katika nchi hii, na hao wanaokaa katika nchi ya Misri. 9#Zab 44:13Naam, nitawatoa watupwe huko na huko katika falme zote za dunia, wapate mabaya; wawe kitu cha kulaumiwa, na mithali, na dhihaka, na laana, katika mahali pote nitakapowafukuza. 10Nami nitatuma upanga, na njaa, na tauni, kati yao, hata watakapopotelea mbali katika nchi niliyowapa, wao na baba zao.

Currently Selected:

Yer 24: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

Videos for Yer 24