YouVersion Logo
Search Icon

Yoe UTANGULIZI

UTANGULIZI
Yoeli, ambaye maana yake ni “BWANA ni Mungu”, hakueleza mengi yamhusuyo yeye binafsi, alipoishi, wala nyakati aliyotoa unabii. Mwanzoni anataja jina la baba yake tu.
Kutokana na unabii wake inakisiwa kuwa alitoa ujumbe huu pale Yerusalemu kabla ya uhamisho wa Babeli. Uwezekano wa pili ni baada ya uhamisho wa Babeli yaani baada ya huduma za Hagai na Zekaria hata baada ya matengenezo ya Ezra na Nehemia (Ezr 5:1-2, 15; Neh 8:1-3, 9; 13:30). Ujumbe wa nabii katika kitabu hiki ni muhimu sana kuliko maisha ya nabii na nyakati za kuandikwa kwake.
Maafa makubwa yaliyosabishwa na nzige na ukame Yuda yanatafasiriwa kuwa ni hukumu ya Mungu kwa Yuda kwa sababu ya dhambi za watu wake. Hata hivyo, iwapo watu watafunga na kutubu, Mungu atawahurumia na kuwabariki upya kwa kuwapa heri tena ndiposa kuna “Siku ya BWANA” (1:15; 2:1,11,31; 3:14). Ujumbe mkuu hapa ni kuwa Mungu atawamiminia watu wote roho yake, rika zote na jinsia zote. Unabii huu wa Yoeli umefasiriwa kuwa ni utabiri wa siku ya Pentekoste (Mdo 2:16-21).
Yaliyomo:
1. Maafa makuu ya nzige, Sura 1:2–2:17
2. Mungu huwahurumia wanaotubu, Sura 2:18–2:27
3. Siku ya Bwana, Sura 2:28–3:21
(a) Kumiminwa Roho (2:28-32)
(b) Hukumu kwa mataifa (3:1-16)
(c) Baraka kwa watu wake (3:17-21)

Currently Selected:

Yoe UTANGULIZI: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in