YouVersion Logo
Search Icon

Yos 4

4
Mawe Kumi na Mawili Yasimamishwa pale Gilgali
1 # Kum 27:2; Yos 3:17 Ikawa, hapo hilo taifa zima lilipokuwa limekwisha vuka Yordani, ndipo BWANA akanena na Yoshua, akamwambia, 2#Hes 13:2; 34:18; Kum 1:23; Yos 1:4-15; 3:12; 1 Fal 18:31Haya, twaeni watu waume kumi na wawili katika hao watu, kila kabila mtu mmoja, 3kisha uwaamrishe, kusema, Twaeni mawe kumi na mawili, hapo katikati ya Yordani, mahali hapo miguu ya hao makuhani iliposimama imara, mwende nayo mawe hayo, mkayaweke nchi kambini, hapo mtakapolala usiku huu. 4Basi Yoshua akawaita hao watu kumi na wawili, aliokuwa amewaweka tayari tangu hapo, katika wana wa Israeli, kila kabila mtu mmoja; 5naye Yoshua akawaambia, Haya, piteni ninyi mtangulie mbele ya sanduku la BWANA, Mungu wenu, mwende pale katikati ya Yordani, mkatwae kila mtu wenu jiwe moja begani mwake, kwa kadiri ya hesabu ya kabila za wana wa Israeli; 6#Kut 12:26; 13:14; Kum 6:20; Zab 44:1; 78:3-6; Isa 38:16ili kwamba jambo hili liwe ishara kati yenu, hapo watoto wenu watakapowauliza ninyi katika siku zijazo, wakisema, Ni nini maana yake mawe haya? 7#Yos 3:13; Kut 12:14; Hes 16:40; 1 Kor 11:24Ndipo mtakapowaambia, Ni kwa sababu maji ya Yordani yalitindika mbele ya sanduku la agano la BWANA; hapo lilipovuka Yordani, hayo maji ya Yordani yalitindika; na mawe haya yatakuwa ni ukumbusho kwa wana wa Israeli milele. 8Basi wana wa Israeli walifanya vile vile kama Yoshua alivyowaamuru, nao wakatwaa mawe kumi na mawili pale katikati ya Yordani, kama BWANA alivyomwambia Yoshua, sawasawa na hesabu ya kabila za wana wa Israeli; wakayachukua wakavuka nayo hata mahali pale walipolala, nao wakayaweka nchi kuko huko. 9#Mwa 28:18; Yos 24:27; 1 Sam 7:12Kisha Yoshua akapanga mawe kumi na mawili katikati ya Yordani, mahali pale miguu ya hao makuhani waliolichukua hilo sanduku la agano iliposimama; nayo yapo pale pale hata hivi leo. 10Kwa kuwa makuhani waliolichukua hilo sanduku walisimama katikati ya Yordani, hata mambo yote BWANA aliyomwamuru Yoshua awambie hao watu yakaisha, sawasawa na hayo yote Musa aliyokuwa amemwamuru Yoshua; kisha hao watu wakafanya haraka wakavuka. 11Ikawa watu wote walipokuwa wamekwisha vuka kabisa, hilo sanduku la BWANA likavuka, na hao makuhani, mbele ya macho ya hao watu. 12#Hes 32:20Na wana wa Reubeni, na wana wa Gadi na hiyo nusu ya kabila ya Manase, wakavuka, hali ya kuvaa silaha mbele ya wana wa Israeli, kama Musa alivyowaambia; 13walipata kama watu arobaini elfu hesabu yao, wenye kuvaa silaha tayari kwa vita, waliovuka mbele ya BWANA, waende vitani, hata nchi tambarare za Yeriko. 14#Yos 3:7; 1 Sam 2:30; 1 Nya 29:12,25; 2 Nya 1:1; 32:23Siku ile BWANA alimtukuza Yoshua mbele ya macho ya Israeli wote; nao wakamcha, kama walivyokuwa wakimcha Musa, siku zote za maisha yake.
15Kisha BWANA akanena na Yoshua, akamwambia, 16#Kut 25:16; Ufu 11:19; Yos 3:15Haya, uwaamuru makuhani, hao waliolichukua sanduku la ushuhuda, kwamba wakwee juu kutoka mle katika Yordani. 17Basi Yoshua akawaamuru hao makuhani, akawaambia, Haya, kweeni mtoke Yordani. 18Ilikuwa, hapo hao makuhani waliolichukua sanduku la agano la BWANA walipokwea juu kutoka mle kati ya Yordani, na nyayo za miguu yao hao makuhani zilipoinuliwa na kutiwa katika nchi kavu, ndipo maji ya Yordani yaliporudi mahali pake, na kujaa na kuipita mipaka yake, kama yalivyokuwa hapo kwanza.
19 # Yos 5:9; 15:7; 1 Sam 11:14,15; Amo 4:4; 5:5; Mik 6:5 Na hao watu wakakwea kutoka Yordani siku ya kumi ya mwezi wa kwanza, wakapiga kambi Gilgali, katika mpaka wa mashariki wa Yeriko. 20Na yale mawe kumi na mawili waliyoyatwaa katikati ya Yordani Yoshua akayasimamisha Gilgali. 21Akawaambia wana wa Israeli, akasema, Watoto wenu watakapowauliza baba zao katika siku zijazo, wakisema, Mawe haya maana yake ni nini? 22Ndipo mtakapowaarifu watoto wenu mkisema, Israeli walivuka mto huu wa Yordani, kwa njia ya nchi kavu. 23#Kut 14:21; Neh 9:11; Zab 77:16,19; 78:13; Isa 43:16; 63:12Kwa sababu BWANA, Mungu wenu aliyakausha maji ya Yordani, mbele yenu, hata mlipokwisha kuvuka kama BWANA, Mungu wenu, alivyoitenda Bahari ya Shamu, aliyoikausha mbele yetu hata tulipokwisha kuvuka; 24#Kut 9:16; Kum 28:10; 1 Sam 17:46; 1 Fal 8:42; 2 Fal 5:15; 19:19; Zab 89:7; 106:8; Yer 32:40; Dan 3:26-29; Kut 15:16; 1 Nya 29:12; Kut 14:31; Kum 6:2; Zab 76:6-8; Yer 10:7watu wote wa duniani wapate kujua mkono wa BWANA, ya kuwa ni mkono wenye uweza, ili wamche BWANA, Mungu wenu, milele.

Currently Selected:

Yos 4: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in