YouVersion Logo
Search Icon

Mt 4

4
Majaribu ya Yesu
1 # Mk 1:12,13; Lk 4:1-13 # Ebr 2:18; 4:15 Kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani, ili ajaribiwe na Ibilisi. 2#Kut 34:28; 1 Fal 19:8Akafunga siku arobaini mchana na usiku, mwisho akaona njaa. 3#Mwa 3:1-7Mjaribu akamjia akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe haya yawe mikate. 4#Kum 8:3Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu. 5#Mt 27:53Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mji mtakatifu, akamweka juu ya kinara cha hekalu, 6#Zab 91:11-12akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu jitupe chini; kwa maana imeandikwa,
Atakuagizia malaika zake;
Na mikononi mwao watakuchukua;
Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.
7 # Kum 6:16 Yesu akamwambia, Tena imeandikwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako. 8Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake, 9akamwambia, Haya yote nitakupa, ukianguka kunisujudia. 10#Kum 6:13Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani; kwa maana imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake. 11#Yn 1:51; Ebr 1:6,14Kisha Ibilisi akamwacha; na tazama, wakaja malaika wakamtumikia.
Yesu Aanza Huduma yake katika Galilaya
12 # Mk 1:14,15; Lk 4:14,15 # Mt 14:3; Mk 6:17; Lk 3:19-20 Basi Yesu aliposikia ya kwamba Yohana amefungwa, alikwenda zake mpaka Galilaya; 13#Yn 2:12akatoka Nazareti, akaja akakaa Kapernaumu, mji ulioko pwani, mipakani mwa Zabuloni na Naftali; 14#Isa 8:13; 9:1ili litimie neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema,
15 # Isa 8:22—9:1 Nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali,
Njia ya bahari, ng’ambo ya Yordani,
Galilaya ya mataifa,
16Watu wale waliokaa katika giza
Wameona mwanga mkuu,
Nao waliokaa katika nchi na uvuli wa mauti
Mwanga umewazukia.
17 # Mt 3:2 Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.
Yesu Awaita Wanafunzi wa Kwanza
18 # Mk 1:16-20; Lk 5:1-11 Naye alipokuwa akitembea kando ya bahari ya Galilaya, aliona ndugu wawili, Simoni aitwaye Petro, na Andrea nduguye, wakitupa jarife baharini; kwa maana walikuwa wavuvi. #Yn 1:40 19#Mt 13:47; Eze 47:10Akawaambia, Nifuateni, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu. 20#Mt 19:27Mara wakaziacha nyavu zao, wakamfuata. 21Akaendelea mbele, akaona ndugu wengine wawili, Yakobo wa Zebedayo, na Yohana nduguye, ambao walikuwamo chomboni pamoja na Zebedayo baba yao, wakizitengeneza nyavu zao; akawaita. 22Mara wakakiacha chombo na baba yao, wakamfuata.
Yesu Awahudumia Makundi ya Watu
23 # Mt 9:35; Mk 1:39; Lk 4:15,44; Mdo 10:38 Naye alikuwa akizunguka katika Galilaya yote, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri Habari Njema ya ufalme, na kuponya ugonjwa na udhaifu wa kila namna katika watu. 24#Mk 6:55Na habari zake zikaenea katika Shamu yote; wakamletea wote waliokuwa hawawezi, walioshikwa na maradhi mbalimbali na mateso, wenye pepo, na wenye kifafa, na wenye kupooza; akawaponya. 25#Mk 3:7,8; Lk 6:17-19Na makutano mengi wakamfuata, kutoka Galilaya, na Dekapoli, na Yerusalemu, na Uyahudi, na ng’ambo ya Yordani

Currently Selected:

Mt 4: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in