YouVersion Logo
Search Icon

Zab 114

114
Maajabu ya Mungu Wakati wa kutoka Misri
1 # Kut 12:51 Haleluya.
Israeli alipotoka Misri,
Na Yakobo katika watu wa lugha ya kigeni.
2Yuda ilikuwa patakatifu pake,
Israeli milki yake.
3 # Kut 14:21; Yos 3:16 Bahari iliona ikakimbia,
Yordani ilirudishwa nyuma.
4 # Zab 29:6; 68:16; Hab 3:6 Milima iliruka kama kondoo waume,
Vilima kama wana-kondoo.
5Ee bahari, una nini, ukimbie?
Yordani, urudi nyuma?
6Enyi milima, mruke kama kondoo waume?
Enyi vilima, kama wana-kondoo?
7Tetemeka, Ee nchi, mbele za uso wa Bwana,
Mbele za uso wa Mungu wa Yakobo.
8 # Kut 17:1-7; Hes 20:2-13; Zab 107:35 Augeuza mwamba kuwa ziwa la maji,
Jiwe gumu kuwa chemchemi.

Currently Selected:

Zab 114: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

Videos for Zab 114