YouVersion Logo
Search Icon

Zab 125

125
Usalama wa Watu wa Mungu
Wimbo wa kupanda mlima.
1Wamtumainio BWANA ni kama mlima Sayuni,
Ambao hautatikisika, wakaa milele.
2Kama milima inavyouzunguka Yerusalemu,
Ndivyo BWANA anavyowazunguka watu wake,
Tangu sasa na hata milele.
3Kwa maana fimbo ya udhalimu
Haitakaa juu ya fungu la wenye haki;
Wenye haki wasije wakainyosha
Mikono yao kwenye upotovu.
4Ee BWANA, uwatendee mema walio wema,
Nao walio wanyofu wa moyo.
5 # Mit 2:15; Isa 59:8; Flp 2:15; Gal 6:16 Bali wao wanaozigeukia njia zao zilizopotoka,
BWANA atawaondoa pamoja na watenda maovu.
Amani ikae na Israeli.

Currently Selected:

Zab 125: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

Videos for Zab 125