YouVersion Logo
Search Icon

Zab 137

137
Maombolezo juu ya Maangamizi ya Yerusalemu
1 # Eze 1:1; Dan 8:2; Isa 24:8; Omb 5:15; Amo 8:10; Ufu 18:22 Kando ya mito ya Babeli ndiko tulikoketi,
Tukalia tulipoikumbuka Sayuni.
2Katika miti iliyo katikati yake
Tulivitundika vinubi vyetu.
3Maana huko waliotuchukua mateka
Walitaka tuwaimbie;
Na waliotuonea walitaka furaha;
Tuimbieni baadhi ya nyimbo za Sayuni.
4Tuuimbeje wimbo wa BWANA
Katika nchi ya ugeni?
5Ee Yerusalemu, nikikusahau wewe,
Mkono wangu wa kuume na usahau.
6 # Eze 3:26 Ulimi wangu na ugandamane
Na kaakaa la kinywa changu, nisipokukumbuka.
Nisipoikuza Yerusalemu
Zaidi ya furaha yangu iliyo kuu.
7 # Omb 4:22; Oba 1:10 Ee BWANA, uwakumbuke wana wa Edomu,
Siku ya Yerusalemu.
Waliosema, Bomoeni!
Bomoeni hata misingini!
8 # Isa 13:1; Ufu 18:6 Ee binti Babeli, uliye karibu na kuangamia,
Heri atakayekupatiliza, ulivyotupatiliza sisi.
9Heri yeye atakayewakamata wadogo wako,
Na kuwaseta wao juu ya mwamba.

Currently Selected:

Zab 137: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in