YouVersion Logo
Search Icon

Zab 138

138
Shukrani na Sifa ya Daudi
1 # Zab 119:46 Nitakushukuru kwa moyo wangu wote,
Mbele ya miungu nitakuimbia zaburi.
2 # 1 Fal 8:29; Zab 5:7; Dan 6:10; Yon 2:7; Isa 42:21 Nitasujudu nikilikabili hekalu lako takatifu,
Nitalishukuru jina lako,
Kwa ajili ya fadhili zako na uaminifu wako,
Kwa maana umeikuza ahadi yako,
Kuliko jina lako lote.
3 # 2 Kor 12:9; Zek 10:12 Siku ile niliyokuita uliniitikia,
Ukanifariji nafsi kwa kunitia nguvu.
4Ee BWANA, wafalme wote wa dunia watakushukuru,
Watakapoyasikia maneno ya kinywa chako.
5Naam, wataziimba njia za BWANA,
Kwa maana utukufu wa BWANA ni mkuu.
6 # Mit 3:34; Yak 4:6 Ingawa BWANA yuko juu, amwona mnyenyekevu,
Naye amjua mwenye kujivuna tokea mbali.
7 # Zab 23:3 Nijapokwenda kati ya shida utanihuisha,
Utanyosha mkono juu ya hasira ya adui zangu,
Na mkono wako wa kuume utaniokoa.
8 # Zab 57:2; Flp BWANA atanitimilizia mambo yangu;
Ee BWANA, fadhili zako ni za milele;
Usiziache kazi za mikono yako.

Currently Selected:

Zab 138: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in