YouVersion Logo
Search Icon

Zab 17

17
Sala ya Ukombozi kutoka kwa Watesaji
Ombi la Daudi.
1Ee BWANA, usikie haki, ukisikilize kilio changu,
Utege sikio lako kwa maombi yangu,
Yasiyotoka katika midomo ya hila.
2Hukumu yangu na itoke kwako,
Macho yako na yatazame mambo ya adili.
3 # Ayu 23:10; Yak 3:2 Umenijaribu moyo wangu, umenijilia usiku,
Umenihakikisha usione neno;
Nimenuia kinywa changu kisikose,
4 # Rum 12:2 Mintarafu matendo ya wanadamu;
Kwa neno la midomo yako
Nimejiepusha na njia za wenye jeuri.
5Nyayo zangu zimeshikamana na njia zako,
Hatua zangu hazikuondoshwa.
6Ee Mungu, nimekuita kwa maana utaitika,
Utege sikio lako ulisikie neno langu.
7Dhihirisha fadhili zako za ajabu
Wewe uwaokoaye wanaokukimbilia;
Kwa mkono wako wa kuume
Uwaokoe nao wanaowaondokea.
8 # Kum 32:10 Unilinde kama mboni ya jicho,
Unifiche chini ya uvuli wa mbawa zako;
9Wasinione wasio haki wanaonionea,
Adui za roho yangu wanaonizunguka.
10Wameukaza moyo wako,
Kwa vinywa vyao hutoa majivuno.
11 # 1 Sam 23:26 Sasa wametuzunguka hatua zetu,
Na kuyakaza macho yao watuangushe chini.
12Kama mfano wa simba atakaye kurarua,
Kama mwana-simba aoteaye katika maoteo yake.
13Ee BWANA, usimame, umkabili, umwinamishe,
Kwa upanga wako uniokoe nafsi na mtu mbaya.
14Ee BWANA, kwa mkono wako uniokoe na watu,
Watu wa dunia hii ambao fungu lao li katika maisha haya.
Matumbo yao wayajaza kwa hazina yako,
Hushiba wana, huwaachia watoto wao akiba zao,
15 # Ayu 19:26,27; Kol 1:15 Bali mimi nikutazame uso wako katika haki,
Niamkapo nishibishwe kwa sura yako.

Currently Selected:

Zab 17: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in