Zab 29
29
Sauti ya Mungu katika Dhoruba
Zaburi ya Daudi.
1 #
Zab 96:7-9; 1 Nya 16:28,29 Mpeni BWANA, enyi wana wa Mungu,
Mpeni BWANA utukufu na nguvu;
2Mpeni BWANA utukufu wa jina lake;
Mwabuduni BWANA kwa uzuri wa utakatifu.
3Sauti ya BWANA i juu ya maji;
Mungu wa utukufu alipiga radi;
BWANA yu juu ya maji mengi.
4Sauti ya BWANA ina nguvu;
Sauti ya BWANA ina adhama;
5Sauti ya BWANA yaivunja mierezi;
Naam, BWANA aivunja-vunja mierezi ya Lebanoni;
6 #
Zab 114:4; Kum 3:9 Airusha-rusha kama ndama wa ng’ombe;
Lebanoni na Sirioni kama mwana-nyati.
7Sauti ya BWANA yaipasua miali ya moto;
8 #
Hes 13:26
Sauti ya BWANA yalitetemesha jangwa;
BWANA alitetemesha jangwa la Kadeshi.
9Sauti ya BWANA yawazalisha ayala,
Na kuifichua misitu;
Na ndani ya hekalu lake
Wanasema wote, Utukufu.
10 #
Zab 93:4
BWANA aliketi juu ya Gharika;
Naam, BWANA ameketi hali ya mfalme milele.
11 #
Isa 40:29
BWANA atawapa watu wake nguvu;
BWANA atawabariki watu wake kwa amani.
Currently Selected:
Zab 29: SUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.