Zab 32
32
Shangwe kwa Kusamehewa
Ya Daudi. Funzo
1 #
Rum 4:7-8; Zab 85:2 Heri aliyesamehewa dhambi,
Na kusitiriwa makosa yake.
2 #
Law 17:4; Rum 5:13; Yn 1:47; 2 Kor 1:12 Heri BWANA asiyemhesabia upotovu,
Ambaye rohoni mwake hamna hila.
3Niliponyamaza mifupa yangu ilichakaa
Kwa kuugua kwangu mchana kutwa.
4Kwa maana mchana na usiku
Mkono wako ulinilemea.
Jasho langu likakauka hata nikawa
Kama nchi kavu wakati wa kaskazi.
5 #
Mit 28:13; Isa 65:24; Lk 15:18 Nalikujulisha dhambi yangu,
Wala sikuuficha upotovu wangu.
Nalisema, Nitayakiri maasi yangu kwa BWANA,
Nawe ukanisamehe upotovu wa dhambi yangu.
6 #
1 Tim 1:16; Isa 55:6; Yn 7:34 Kwa hiyo kila mtu mtauwa
Akuombe wakati unapopatikana.
Hakika maji makuu yafurikapo,
Hayatamfikia yeye.
7 #
Zab 9:9; Mit 18:10; Isa 4:6; Mt 23:37; Kol 3:3 Ndiwe sitara yangu, utanihifadhi na mateso,
Utanizungusha nyimbo za wokovu.
8 #
Isa 48:17
Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea;
Nitakushauri, jicho langu likikutazama.
9Msiwe kama farasi wala nyumbu,
Walio hawana akili.
Kwa matandiko ya lijamu na hatamu
Sharti kuwazuia hao, au hawatakukaribia.
10 #
Mit 13:21; Zab 34:8; Mit 16:20; Yer 17:7 Naye mtu mwovu ana mapigo mengi,
Bali amtumainiye BWANA fadhili zitamzunguka.
11Mfurahieni BWANA;
Shangilieni, enyi wenye haki
Pigeni vigelegele vya furaha;
Ninyi nyote mlio wanyofu wa moyo.
Currently Selected:
Zab 32: SUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.