Zab 42
42
KITABU CHA PILI
Hamu ya Kusaidiwa na Mungu katika Dhiki
Kwa mwimbishaji. Utenzi wa Wakorahi.
1Kama ayala aioneavyo shauku mito ya maji.
Vivyo hivyo nafsi yangu inakuonea shauku, Ee Mungu.
2 #
Yn 7:37; 1 The 1:9 Nafsi yangu inamwonea kiu MUNGU, Mungu aliye hai,
Lini nitakapokuja nionekane mbele za Mungu?
3Machozi yangu yamekuwa chakula changu mchana na usiku,
Pindi wanaponiambia mchana kutwa, Yuko wapi Mungu wako.
4 #
Isa 30:29
Nayakumbuka hayo nikiweka wazi nafsi yangu ndani yangu,
Jinsi nilivyokuwa nikienda na mkutano,
Na kuwaongoza nyumbani kwa Mungu,
Kwa sauti ya furaha na kusifu, mkutano wa sikukuu.
5 #
Zab 56:3,11; Isa 50:10; Omb 3:24 Nafsi yangu, kwa nini kuinama,
Na kufadhaika ndani yangu?
Umtumaini Mungu;
Kwa maana nitakuja kumsifu,
Aliye afya ya uso wangu,
Na Mungu wangu.
6Nafsi yangu imeinama ndani yangu, kwa hiyo nitakukumbuka,
Toka nchi ya Yordani, na Mahermoni, na toka kilima cha Mizari.
7 #
Eze 7:26
Kilindi chapigia kelele kilindi kwa sauti ya maboromoko ya maji yako,
Gharika zako zote na mawimbi yako yote yamepita juu yangu.
8 #
Kum 28:8
Mchana BWANA ataagiza fadhili zake, na usiku wimbo wake utakuwa nami,
Naam, maombi kwa Mungu aliye uhai wangu.
9Nitamwambia Mungu, mwamba wangu, Kwa nini umenisahau?
Kwa nini ninakwenda nikihuzunika, adui wakinionea?
10Watesi wangu hunitukana mithili ya kuniponda mifupa yangu,
Pindi wanaponiambia mchana kutwa, Yuko wapi Mungu wako?
11Nafsi yangu, kwa nini kuinama,
Na kufadhaika ndani yangu?
Umtumaini Mungu;
Kwa maana nitakuja kumsifu,
Aliye afya ya uso wangu,
Na Mungu wangu.
Currently Selected:
Zab 42: SUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.