YouVersion Logo
Search Icon

Zab 48

48
Utukufu wa Nguvu za Sayuni
Wimbo. Zaburi ya Wakorahi.
1 # Isa 2:2; Oba 1:17; Mik 4:1 Bwana ndiye aliye mkuu,
Na mwenye kusifiwa sana.
Katika mji wa Mungu wetu,
Katika mlima wake mtakatifu.
2 # Mt 5:35; Yer 3:19; Omb 2:15; Eze 20:6; Isa 14:13 Kuinuka kwake ni mzuri sana,
Ni furaha ya dunia yote.
Mlima Sayuni pande za kaskazini,
Mji wa Mfalme mkuu.
3Mungu katika majumba yake
Amejijulisha kuwa ngome.
4 # 2 Sam 10:6 Maana, tazama, wafalme walikusanyika;
Walipita wote pamoja.
5Waliona, mara wakashangaa;
Wakafadhaika na kukimbia.
6Papo hapo tetemeko liliwashika,
Utungu kama wa mwanamke azaaye.
7 # Eze 27:26 Kwa upepo wa mashariki
Wavunja jahazi za Tarshishi.
8 # Isa 2:2; Mik 4:1 Kama tulivyosikia, ndivyo tulivyoona,
Katika mji wa BWANA wa majeshi.
Mji wa Mungu wetu;
Mungu ataufanya imara hata milele.
9Tumezitafakari fadhili zako, Ee Mungu,
Katikati ya hekalu lako.
10 # Mal 1:11 Kama lilivyo jina lako, Ee Mungu,
Ndivyo na sifa yako hata miisho ya dunia.
Mkono wako wa kuume umejaa haki;
11Na ufurahi mlima Sayuni.
Binti za Yuda na washangilie
Kwa sababu ya hukumu zako.
12Tembeeni katika Sayuni,
Uzungukeni mji,
Ihesabuni minara yake,
13Tieni moyoni boma zake,
Yafikirini majumba yake,
Mpate kuwaambia kizazi kitakachokuja.
14 # Isa 25:9 Kwa maana ndivyo alivyo
MUNGU, Mungu wetu.
Milele na milele
Yeye ndiye atakayetuongoza.

Currently Selected:

Zab 48: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

Videos for Zab 48