Zab 52
52
Hukumu kwa Waongo
Kwa mwimbishaji. Utenzi wa Daudi, wakati Doegi, Mwedomu alipomwendea Sauli na kumwambia, “Daudi ameingia nyumbani mwa Ahimeleki.”
1 #
1 Sam 22:9-10; 21:7 Kwa nini kujisifia uovu, Ewe jabari?
Wema wa Mungu upo sikuzote.
2 #
Zab 50:19; Mit 12:18; Zab 59:7 Ulimi wako watunga madhara,
Kama wembe mkali, Ewe mwenye hila
3 #
Yer 9:4
Umependa mabaya kuliko mema,
Na uongo kuliko kusema kweli.
4Umependa maneno yote ya kupoteza watu,
Ewe ulimi wenye hila.
5 #
Mit 2:22
Lakini Mungu atakuharibu hata milele;
Atakuondolea mbali;
Atakunyakua hemani mwako;
Atakung’oa katika nchi ya walio hai.
6 #
Ayu 22:19; Zab 58:10 Nao wenye haki wataona;
Wataingiwa na hofu na kumcheka;
7 #
Ayu 31:24,25; Zab 49:6 Kumbe! Huyu ndiye mtu yule,
Asiyemfanya Mungu kuwa nguvu zake.
Aliutumainia wingi wa mali zake,
Na kujifanya hodari kwa madhara yake.
8 #
Zab 92:13
Bali mimi ni kama mzeituni
Umeao katika nyumba ya Mungu.
Nazitumainia fadhili za Mungu milele na milele.
9 #
Zab 54:6
Nitakushukuru milele kwa maana umetenda;
Nitalingojea jina lako kwa kuwa ni jema;
Mbele ya wacha Mungu wako.
Currently Selected:
Zab 52: SUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.