YouVersion Logo
Search Icon

Zab 59

59
Sala ya Kuponywa kutoka Adui
Kwa mwimbishaji: kwa mtindo wa Usiharibu. Utenzi wa Daudi, wakati Sauli alipowaagiza wapelelezi waende nyumbani mwake ili wamuue.
1Ee Mungu wangu, uniponye na adui zangu,
Uniinue juu yao wanaoshindana nami.
2Uniponye nao wafanyao maovu,
Uniokoe na watu wa damu.
3 # 1 Sam 26:18 Kwa maana wanaiotea nafsi yangu;
Wenye nguvu wamenikusanyikia;
Ee BWANA, si kwa kosa langu,
Wala si kwa hatia yangu.
4Bila kosa langu huenda mbio, hujiweka tayari;
Uamke uonane nami, na kutazama.
5 # Dan 4:35 Na Wewe, BWANA, Mungu wa majeshi,
Mungu wa Israeli, uamke.
Uwapatilize mataifa yote;
Usiwarehemu waovu wafanyao uovu hata mmoja.
6Wakati wa jioni hurudi, hulia kama mbwa,
Na kuzunguka-zunguka mjini.
7Tazama, kwa vinywa vyao huteuka,
Midomoni mwao mna panga,
Kwa maana ni nani asikiaye?
8 # Zab 2:4; Mit 1:26 Na Wewe, BWANA, utawacheka,
Utawadhihaki mataifa yote.
9Ee nguvu zangu, nitakungoja Wewe,
Maana Mungu ndiye aliye ngome yangu
10Mungu wa fadhili zangu atanitangulia,
Mungu atanijalia kuwatazama adui zangu.
11 # Mwa 4:12,13 Usiwaue, watu wangu wasije wakasahau;
Uwatawanye kwa uweza wako,
Na kuwaangamiza, Ee Bwana, ngao yetu.
12Kwa dhambi ya kinywa chao,
Na kwa neno la midomo yao,
Wanaswe kwa kiburi chao,
Kwa ajili ya kulaani na uongo wasemao.
13Uwakomeshe kwa hasira,
Uwakomeshe watoweke,
Wajue ya kuwa Mungu atawala katika Yakobo,
Na hata miisho ya dunia.
14Wakati wa jioni hurudi, hulia kama mbwa,
Na kuzunguka-zunguka mjini.
15Watatanga-tanga hao wakitafuta chakula;
Wasiposhiba watakesha usiku kucha.
16Nami nitaziimba nguvu zako asubuhi,
Nitaziimba fadhili zako kwa furaha.
Kwa kuwa ndiwe uliyekuwa ngome yangu,
Na makimbilio siku ya shida yangu.
17Ee nguvu zangu, nitakuimbia kwa furaha,
Maana Mungu ndiye aliye ngome yangu,
Mungu wa fadhili zangu.

Currently Selected:

Zab 59: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

Videos for Zab 59