YouVersion Logo
Search Icon

Zab 77

77
Matendo Makuu ya Mungu Yasimuliwa
Kwa mwimbishaji: kwa kufuata Yeduthuni. Ya Asafu. Zaburi.
1Nimpazie Mungu sauti yangu,
Naam, nimpazie Mungu, naye atanisikia.
2 # Zab 50:15; Isa 26:9 Siku ya taabu yangu nalimtafuta Bwana;
Mkono wangu ulinyoshwa usiku, haukulegea;
Nafsi yangu ilikataa kufarijika.
3Nilipotaka kumkumbuka Mungu nalifadhaika;
Nilipotaka kutafakari roho yangu ilizimia.
4Ulizishika kope za macho yangu zisifumbike;
Naliona mashaka nisiweze kunena.
5 # Kum 32:7; Zab 14:5; Isa 51:9 Nalifikiri habari za siku za kale,
Miaka ya zamani zilizopita.
6Nakumbuka wimbo wangu usiku,
Nawaza moyoni mwangu,
Roho yangu ikatafuta.
7Je! Bwana atatupa milele na milele?
Hatatenda fadhili tena kabisa?
8 # Isa 27:11; Yon 2:4; Hes 23:19; Yer 15:18; Rum 9:6 Rehema zake zimekoma hata milele?
Ahadi yake imekwisha hata vizazi vyote?
9 # Isa 49:15 Mungu amesahau fadhili zake?
Amezuia kwa hasira rehema zake?
10 # Ayu 42:3; Zab 31:22; Yer 10:19 Nikasema, Ndio udhaifu wangu huo;
Lakini nitaikumbuka miaka ya mkono wa kuume wake Aliye juu.
11 # 1 Nya 16:12; Zab 28:5; Isa 5:1 Nitayakumbuka matendo ya BWANA;
Naam, nitayakumbuka maajabu yako ya kale.
12Pia nitaitafakari kazi yako yote;
Nitaziwaza habari za matendo yako.
13 # Zab 73:17 Ee Mungu, njia yako i katika utakatifu;
Ni nani aliye mungu mkuu kama Mungu?
14Wewe ndiwe Mungu ufanyaye maajabu;
Uliudhihirisha uweza wako kati ya mataifa.
15Kwa mkono wako umewakomboa watu wako,
Wana wa Yakobo na Yusufu.
16 # Kut 14:21; Yos 3:15,16 Ee Mungu, yale maji yalikuona,
Yale maji yalikuona, yakaogopa.
Vilindi vya maji navyo vikatetemeka,
17Mawingu yakamwaga maji.
Mbingu nazo zikatoa sauti,
Mishale yako nayo ikatapakaa.
18Sauti ya radi yako ikawa katika kisulisuli;
Umeme uliuangaza ulimwengu.
Nchi ilitetemeka na kutikisika;
19 # Hab 3:15; Kut 14:28; Ayu 37:23 Njia yako ilikuwa katika bahari.
Na mapito yako yalikuwa katika maji makuu;
Hatua zako hazikujulikana.
20 # Isa 63:11 Uliwaongoza watu wako kama kundi,
Kwa mkono wa Musa na Haruni.

Currently Selected:

Zab 77: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

Videos for Zab 77