YouVersion Logo
Search Icon

Ufu 8

8
Mhuri wa Saba na Chetezo cha Dhahabu
1 # Zek 2:13; Hab 2:20 Hata alipoifungua muhuri ya saba, kukawa kimya mbinguni kama muda wa nusu saa. 2#Mt 24:31Nami nikawaona wale malaika saba wasimamao mbele za Mungu, nao wakapewa baragumu saba. 3#Amo 9:1; Kut 30:1,3; Ufu 5:8Na malaika mwingine akaja akasimama mbele ya madhabahu, mwenye chetezo cha dhahabu, akapewa uvumba mwingi, ili autie pamoja na maombi ya watakatifu wote juu ya madhabahu ya dhahabu, iliyo mbele ya kiti cha enzi. 4#Zab 141:2Na moshi wa ule uvumba ukapanda mbele za Mungu pamoja na maombi ya watakatifu, kutoka mkononi mwa malaika. 5#Law 16:12; Eze 10:2; Kut 19:16; Ufu 11:19; 16:18Na huyo malaika akakitwaa kile chetezo, akakijaza moto wa madhabahu, akautupa juu ya nchi, kukawa radi na sauti na umeme na tetemeko la nchi.
6Na wale malaika saba wenye baragumu saba wakajifanya tayari ili wazipige.
7 # Kut 9:23-25; Eze 38:22; Yoe 2:30 Malaika wa kwanza akapiga baragumu, kukawa mvua ya mawe na moto vilivyotangamana na damu, vikatupwa juu ya nchi; theluthi ya nchi ikateketea, na theluthi ya miti ikateketea, na majani mabichi yote yakateketea.
8 # Yer 51:25; Kut 7:20,21 Malaika wa pili akapiga baragumu, na kitu, mfano wa mlima mkubwa uwakao moto, kikatupwa katika bahari; theluthi ya bahari ikawa damu. 9Wakafa theluthi ya viumbe vilivyomo baharini, vyenye uhai; theluthi ya merikebu zikaharibiwa.
10 # Isa 14:12; Dan 8:10 Malaika wa tatu akapiga baragumu, nyota kubwa ikaanguka kutoka mbinguni, iliyokuwa ikiwaka kama taa, ikaanguka juu ya theluthi ya mito, na juu ya chemchemi za maji. 11#Yer 9:14Na jina lake ile nyota yaitwa Pakanga; theluthi ya maji ikawa pakanga, na wanadamu wengi wakafa kwa maji hayo, kwa kuwa yalitiwa uchungu.
12 # Isa 13:10; Eze 32:7; Yoe 2:10,31; 3:15; Ufu 6:12; Kut 10:21 Malaika wa nne akapiga baragumu, theluthi ya jua ikapigwa, na theluthi ya mwezi, na theluthi ya nyota, ili kwamba ile theluthi itiwe giza, mchana usiangaze theluthi yake, wala usiku vivyo hivyo.
13 # Ufu 9:12; 11:14 Kisha nikaona, nikasikia tai mmoja akiruka katikati ya mbingu, akisema kwa sauti kuu, Ole, ole, ole wao wakaao juu ya nchi! Kwa sababu ya sauti zisaliazo za baragumu za malaika watatu, walio tayari kupiga.

Currently Selected:

Ufu 8: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in