Tit 3
3
Dumisha Matendo Mema
1 #
1 Pet 2:13
Uwakumbushe watu kunyenyekea kwa wenye uwezo na mamlaka, na kutii, na kuwa tayari kwa kila kazi njema; 2#Flp 4:5wasimtukane mtu ye yote, wasiwe wagomvi, wawe wema, wakionyesha upole wote kwa watu wote. 3#1 Kor 6:11; Efe 2:2; 5:8Maana hapo zamani sisi nasi tulikuwa hatuna akili, tulikuwa waasi, tumedanganywa, huku tukitumikia tamaa na anasa za namna nyingi, tukiishi katika uovu na husuda, tukichukiza na kuchukiana. 4#Tit 2:11; Mit 8:31Lakini wema wake Mwokozi wetu Mungu, na upendo wake kwa wanadamu, ulipofunuliwa, alituokoa; 5#Efe 2:8,9; 5:26; Yn 3:5; 2 Tim 1:9si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu; 6#Yoe 2:28ambaye alitumwagia kwa wingi, kwa njia ya Yesu Kristo Mwokozi wetu; 7#Rum 3:24ili tukihesabiwa haki kwa neema yake, tupate kufanywa warithi wa uzima wa milele, kama lilivyo tumaini letu. 8Ni neno la kuaminiwa; na mambo hayo nataka uyanene kwa nguvu, ili wale waliomwamini Mungu wakumbuke kudumu katika matendo mema. Hayo ni mazuri, tena yana faida kwa wanadamu. 9#1 Tim 4:7Lakini maswali ya upuzi ujiepushe nayo, na nasaba, na magomvi, na mashindano ya sheria. Kwa kuwa hayana faida, tena hayana maana. 10#2 Yoh 1:10; Mt 18:15,16Mtu aliye mzushi, baada ya kumwonya mara ya kwanza na mara ya pili, mkatae; 11#1 Tim 6:4,5ukijua ya kuwa mtu kama huyo amepotoka, tena atenda dhambi, maana amejihukumu hatia yeye mwenyewe.
Ujumbe wa Mwisho na Baraka
12 #
2 Tim 4:12
Wakati nitakapomtuma Artema kwako au Tikiko, jitahidi kuja kwangu huku Nikopoli; kwa maana huku nimekusudia kukaa wakati wa baridi. 13#Mdo 18:24; 1 Kor 3:5,6Zena, yule mwana-sheria, na Apolo, uwasafirishe kwa bidii, wasipungukiwe na cho chote. 14#Tit 2:14; Mt 7:19; Efe 4:28,29Watu wetu nao wajifunze kudumu katika matendo mema, kwa matumizi yaliyo lazima, ili wasiwe hawana matunda.
15Watu wote walio pamoja nami wakusalimu. Tusalimie wale watupendao katika imani.
Neema na iwe pamoja nanyi nyote.
Currently Selected:
Tit 3: SUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.