Yohana 18
18
Kusalitiwa na kukamatwa kwa Yesu
1 #
Mt 26:36; Mk 14:32; Lk 22:39; 2 Sam 15:23 Alipokwisha kusema hayo, Yesu alitoka pamoja na wanafunzi wake kwenda ng'ambo ya kijito Kedroni, palipokuwapo bustani; akaingia yeye na wanafunzi wake. 2#Mt 26:47-56; Mk 14:43-52; Lk 22:47-53 Naye Yuda, yule aliyetaka kumsaliti, alipajua mahali pale; kwa sababu Yesu alikuwa akienda huko mara nyingi pamoja na wanafunzi wake. #Lk 21:37 3Basi Yuda, akiisha kupokea kikosi cha askari na watumishi waliotoka kwa wakuu wa makuhani na Mafarisayo, akaenda huko na taa na mienge na silaha. 4#Yn 19:28 Basi Yesu, huku akijua yote yatakayompata, akatokea, akawaambia, Ni nani mnayemtafuta? 5Wao wakamjibu, Ni Yesu Mnazareti. Yesu akawaambia, Ni mimi. Yuda naye aliyemsaliti alikuwa amesimama pamoja nao. 6Basi alipowaambia, Ni mimi, walirudi nyuma, wakaanguka chini. 7Basi akawauliza tena, Mnamtafuta nani? Wakasema, Yesu Mnazareti. 8Yesu akajibu, Nimekwisha kuwaambieni ya kwamba ni mimi; basi ikiwa mnanitafuta mimi, waacheni hawa waende zao. 9#Yn 17:12 Ili litimizwe lile neno alilolisema, Wale ulionipa sikumpoteza hata mmoja wao. 10Basi Simoni Petro alikuwa na upanga, akaufuta, akampiga mtumwa wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio la kulia. Na yule mtumwa jina lake ni Malko. 11#Mt 26:39; Mk 14:36; Lk 22:42 Basi Yesu akamwambia Petro, Rudisha upanga alani mwake; je! Kikombe alichonipa Baba, mimi nisikinywee?
Yesu mbele ya kuhani mkuu
12 #
Mt 26:57-75; Mk 14:53-72; Lk 22:54-71 Basi wale askari na yule jemadari na wale watumishi wa Wayahudi walimkamata Yesu, wakamfunga. 13Wakampeleka kwa Anasi kwanza; maana alikuwa baba mkwe wa Kayafa, yule aliyekuwa Kuhani Mkuu mwaka ule. 14#Yn 11:49-50 Naye Kayafa ndiye yule aliyewapa Wayahudi lile shauri ya kwamba yafaa mtu mmoja afe kwa ajili ya watu.
Petro amkana Yesu
15 #
Yn 20:3; 21:20; Mdo 3:1 Wakamfuata Yesu, Petro na mwanafunzi mwingine. Na mwanafunzi huyo alikuwa amejulikana na Kuhani Mkuu, akaingia pamoja na Yesu katika ukumbi wa Kuhani Mkuu. 16Lakini Petro akasimama nje mlangoni. Basi yule mwanafunzi mwingine aliyejulikana na Kuhani Mkuu akatoka, akasema na mlinda mlango, akamleta Petro ndani. 17Basi yule kijakazi, aliyekuwa mlinda mlango, akamwambia Petro, Wewe nawe, je! Hu mwanafunzi mmojawapo wa mtu huyu? Naye akasema, Si mimi. 18Na wale watumwa na watumishi walikuwa wakisimama, wamewasha moto wa makaa; maana kulikuwa na baridi; wakawa wakiota moto. Petro naye alikuwapo pamoja nao, anaota moto.
Kuhani Mkuu amhoji Yesu
19Basi Kuhani Mkuu akamwuliza Yesu kuhusu wanafunzi wake, na kuhusu mafundisho yake. 20#Yn 7:14,26; Mt 10:27 Yesu akamjibu, Mimi nimesema na ulimwengu waziwazi; sikuzote nilifundisha katika sinagogi na katika hekalu, wakusanyikapo Wayahudi wote; wala mimi sikusema neno lolote kwa siri. 21Ya nini kuniuliza mimi? Waulize wale waliosikia ni nini niliyowaambia; wao wanajua niliyoyanena. 22#Yn 19:3; Mdo 23:2 Basi aliposema hayo, mtumishi mmojawapo aliyesimama karibu alimpiga Yesu kofi akisema, Wamjibu hivi Kuhani Mkuu? 23Yesu akamjibu, Kama nimesema vibaya, ushuhudie ule ubaya; bali kama nimesema vema, wanipigia nini? 24Basi Anasi akampeleka akiwa amefungwa kwa Kayafa, Kuhani Mkuu.
Petro amkana tena Yesu mara ya pili
25Na Simoni Petro alikuwa akisimama huko, anakota moto. Basi wakamwambia, Wewe nawe, je! Hu mwanafunzi wake mmojawapo? Naye akakana, akasema, Si mimi. 26Mtumwa mmojawapo wa Kuhani Mkuu, naye ni jamaa yake yule aliyekatwa sikio na Petro, akasema, Je! Mimi sikukuona wewe bustanini pamoja naye? 27Basi Petro akakana tena, na mara jogoo akawika.
28 #
Mt 27:2,11-30; Mk 15:1-19; Lk 23:1-25 Kisha wakamchukua Yesu kutoka kwa Kayafa mpaka Praitorio,#18:28 Praitorio: maana ni Nyumba ya Uliwali. nayo ikawa alfajiri; lakini wao wenyewe hawakuingia ndani ya ile Praitorio, wasije wakanajisika, bali wapate kuila Pasaka. 29Basi Pilato akawatokea nje, akasema, Ni mashitaka gani mnayoleta juu ya mtu huyu? 30Wakajibu, wakamwambia, Kama huyu asingekuwa mtenda mabaya, tusingemleta kwako. 31#Yn 19:6,7; Mdo 18:15 Basi Pilato akawaambia, Haya! Mtwaeni ninyi, mkamhukumu kwa ile torati yenu! Wayahudi wakamwambia, Sisi hatuna ruhusa ya kuua mtu. 32#Yn 3:14; 12:32; 19:32,33; Mt 20:19 Ili litimie lile neno lake Yesu alilolisema, akionesha ni mauti gani atakayokufa.
33Basi Pilato akaingia tena ndani ya Praitorio, akamwita Yesu, akamwambia, Je! Wewe ni Mfalme wa Wayahudi? 34#Mt 16:13 Yesu akamjibu, Wewe wasema hivi kwa nafsi yako, au watu wengine walikuambia habari zangu? 35#Yn 1:11; Mt 21:39 Pilato akajibu, Ama! Ni Myahudi mimi! Taifa lako na wakuu wa makuhani ndio waliokuleta kwangu. Umefanya nini? 36Yesu akajibu, Ufalme wangu sio wa ulimwengu huu. Kama ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu, watumishi wangu wangenipigania, nisije nikatiwa mikononi mwa Wayahudi. Lakini ufalme wangu sio wa hapa. 37#1 Tim 6:13; Yn 8:47; 10:27 Basi Pilato akamwambia, Wewe u mfalme basi? Yesu akajibu, Wewe wasema, kwa kuwa mimi ni mfalme. Mimi nimezaliwa kwa ajili ya haya, na kwa ajili ya haya mimi nilikuja ulimwenguni, ili niishuhudie kweli. Kila aliye wa hiyo kweli hunisikia sauti yangu. 38Pilato akamwambia, Kweli ni nini?
Yesu ahukumiwa Kifo
Naye akiisha kusema neno hilo akawatokea Wayahudi tena, akawaambia, Mimi sioni hatia yoyote kwake. 39Lakini kwenu kuna desturi ya mimi kuwafungulia mtu mmoja wakati wa Pasaka; basi, mwapenda niwafungulie Mfalme wa Wayahudi? 40Basi wakapiga kelele tena kusema, Si huyu, bali Baraba. Naye yule Baraba alikuwa mnyang'anyi.
Currently Selected:
Yohana 18: SRUVDC
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.