YouVersion Logo
Search Icon

1 Mambo ya Nyakati 23

23
Familia za Walawi na wajibu wao
1 # 1 Fal 1:33; 1 Nya 28:5; 29:22-25 Basi Daudi alipokuwa mzee kwa kuishi siku nyingi; alimtawaza mwanawe Sulemani awe mfalme wa Waisraeli. 2Akawakusanya wakuu wote wa Israeli, pamoja na makuhani na Walawi. 3#Hes 4:3 Nao wakahesabiwa Walawi wenye miaka thelathini na zaidi; na jumla yao kwa vichwa, mtu kwa mtu, ikawa elfu thelathini na nane. 4#Kum 16:18; 1 Nya 26:29; 2 Nya 19:8 Katika hao elfu ishirini na nne walikuwa wa kusimamia kazi ya nyumba ya BWANA; na elfu sita walikuwa maofisa na waamuzi; 5#2 Nya 29:25,26; Amo 6:5 na elfu nne walikuwa mabawabu; na elfu nne walimsifu BWANA kwa vinanda, nilivyovifanya, alisema Daudi, vya kumsifia. 6#Kut 6:16; Hes 26:57; 1 Nya 6:1; 2 Nya 8:14; 29:25; 31:2; 35:10; Ezr 6:18 Basi Daudi akawagawanya kwa zamu zao sawasawa na wana wa Lawi; Gershoni, Kohathi, na Merari. 7Wa Wagershoni; Ladani, na Shimei. 8Wana wa Ladani; Yehieli mkuu wao, na Zethamu, na Yoeli, watu watatu. 9Wana wa Shimei; Shelomothi, na Hazieli, na Harani, watatu. Hao walikuwa vichwa vya koo za baba za Ladani. 10Na wana wa Shimei; Yahathi, na Zina, na Yeushi, na Beria. Hao wanne walikuwa wana wa Shimei. 11Naye Yahathi alikuwa mkubwa wao, na Zina alikuwa wa pili; lakini Yeushi na Beria hawakuwa na wana wengi; basi wakahesabiwa pamoja kama ukoo mmoja. 12#Kut 6:18; 1 Nya 6:2 Wana wa Kohathi; Amramu, Ishari, Hebroni, na Uzieli, watu wanne. 13#Kut 28:1; Hes 18:1,7; Ebr 5:4; Kut 30:7; Law 10:1,2; Hes 16:40; 1 Sam 2:28; Kum 21:5; Hes 6:23 Wana wa Amramu; Haruni na Musa; naye Haruni akatengwa, ili ayatakase yaliyo matakatifu sana, yeye na wanawe milele, ili kufukiza uvumba mbele za BWANA, kumtumikia, na kubariki kwa jina lake, milele. 14Lakini kwa habari za Musa, mtu wa Mungu, wanawe hutajwa miongoni mwa kabila la Lawi. 15#Kut 2:22; 18:3,4 Wana wa Musa; Gershomu na Eliezeri. 16Wana wa Gershomu; Shebueli mkuu wao. 17Na wana wa Eliezeri; Rehabia mkuu wao. Yeye Eliezeri hakuwa na wana wengine; lakini wana wa Rehabia walikuwa wengi sana. 18Wana wa Ishari; Shelomithi mkuu wao. 19Wana wa Hebroni; Yeria mkuu wao, Amaria wa pili, Yahazieli wa tatu, na Yekameamu wa nne. 20Wana wa Uzieli; Mika mkuu wao, na Ishia wa pili. 21Wana wa Merari; Mali na Mushi. Wana wa Mali; Eleazari, na Kishi. 22#Hes 36:6 Akafa Eleazari, wala hakuwa na wana, ila binti tu; na ndugu zao, wana wa Kishi, wakawaoa. 23#1 Nya 24:30 Wana wa Mushi; Mali, na Ederi, na Yeremothi, watu watatu. 24#Hes 10:17; 1:3; 4:3 Hao walikuwa wana wa Lawi, kwa kufuata koo za baba zao, yaani, vichwa vya koo za baba zao waliohesabiwa, kwa hiyo hesabu ya majina yao, hao walioifanya kazi ya utumishi wa nyumba ya BWANA, wenye miaka ishirini na zaidi. 25Kwa kuwa Daudi alisema, BWANA, Mungu wa Israeli, amewastarehesha watu wake; naye hukaa Yerusalemu milele; 26#Hes 4:5 wala Walawi hawahitaji tena kuichukua maskani, na vyombo vyake vyote kwa utumishi wake. 27Maana kwa maneno ya mwisho ya Daudi, hao wana wa Lawi walihesabiwa, wenye miaka ishirini na zaidi. 28Kwani kazi yao ilikuwa kuwangojea wana wa Haruni katika utumishi wa nyumba ya BWANA, nyuani, na vyumbani, na kwa kuvisafisha vitakatifu vyote, ndiyo kazi ya utumishi wa nyumba ya Mungu; 29#Kut 25:30; Law 24:5-9; 1 Nya 9:29,32; Law 6:20; 2:4; 19:35 tena kazi ya mikate ya wonyesho, na ya unga mwembamba wa sadaka ya unga; ikiwa ni wa maandazi yasiyochachwa, au wa yale yaliyotokoswa, au wa yale yaliyookwa; na kazi ya kila namna ya kipimo na cheo; 30#1 Nya 6:31-33; 9:33; 2 Nya 31:2; Zab 135:1,3,19,20; Ufu 5:8-14; 14:3 nao wasimame kila asubuhi kumshukuru na kumsifu BWANA, na jioni vivyo hivyo; 31#Hes 10:10; Zab 81:3; Isa 1:13,14; Law 23:4 na kumtolea BWANA sadaka zote za kuteketezwa, katika siku za sabato, za mwezi mpya, na za sikukuu zilizoagizwa, kwa hesabu kadiri ya agizo lake, daima mbele za BWANA; 32#Hes 1:53; 3:6 tena ni wajibu wao kuitunza hema ya kukutania na patakatifu na kuwasaidia wana wa Haruni, ndugu zao, katika utumishi wa nyumba ya BWANA.

Currently Selected:

1 Mambo ya Nyakati 23: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

Video for 1 Mambo ya Nyakati 23