YouVersion Logo
Search Icon

1 Wakorintho 1

1
Salamu
1Paulo, aliyeitwa kuwa mtume wa Yesu Kristo kwa mapenzi ya Mungu, na Sosthene ndugu yetu, 2#Mdo 18:1; 1 Kor 6:11; Mdo 9:14 kwa kanisa la Mungu lililoko Korintho, wale waliotakaswa katika Kristo Yesu, walioitwa wawe watakatifu, pamoja na wote wanaoliitia jina la Bwana wetu Yesu Kristo kila mahali, Bwana wao na wetu. 3#Rum 1:7 Neema na iwe kwenu na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu, na kwa Bwana Yesu Kristo.
4Namshukuru Mungu sikuzote kwa ajili yenu, kwa sababu ya neema ya Mungu mliyopewa katika Kristo Yesu; 5kwa kuwa katika kila jambo mlitajirika katika yeye, katika maneno yote, na maarifa yote; 6kama ushuhuda wa Kristo ulivyothibitika kwenu; 7#Lk 17:30; 2 The 1:7; Tit 2:13 hata hamkupungukiwa na karama yoyote, mkikutazamia sana kufunuliwa kwake Bwana wetu Yesu Kristo; 8#Flp 1:6; 1 The 3:13; 5:23 ambaye atawathibitisha hata mwisho, ili msilaumiwe siku ile ya Bwana wetu Yesu Kristo. 9#1 The 5:24; 1 Yoh 1:3 Mungu ni mwaminifu ambaye mliitwa na yeye mwingie katika ushirika wa Mwanawe, Yesu Kristo Bwana wetu.
Migawanyiko katika kanisa
10 # Flp 2:2; 3:16 Basi ndugu, nawasihi, kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba nyote mnene mamoja; wala pasiwe kwenu migawanyiko, bali mhitimu katika nia moja na shauri moja. 11Kwa maana, ndugu zangu, nimearifiwa habari zenu na wale walio wa nyumbani mwa Kloe, ya kwamba uko ugomvi kwenu. 12#Mdo 18:24,27; 1 Kor 3:4; Yn 1:42 Basi, maana yangu ni hii, ya kwamba kila mtu wa kwenu kusema, Mimi ni wa Paulo, na, Mimi ni wa Apolo, na, Mimi ni wa Kefa, na, Mimi ni wa Kristo. 13Je! Kristo amegawanyika? Je! Paulo alisulubiwa kwa ajili yenu? Au je! Mlibatizwa kwa jina la Paulo? 14#Mdo 18:8; 19:29; Rum 16:23 Nashukuru, kwa sababu sikumbatiza mtu kwenu, ila Krispo na Gayo; 15mtu asije akasema kwamba mlibatizwa kwa jina langu. 16#1 Kor 16:15 Tena niliwabatiza watu wa nyumbani mwa Stefana; zaidi ya hao, sijui kama nilimbatiza mtu yeyote mwingine. 17#Yn 4:2; Mt 28:19 Maana Kristo hakunituma ili nibatize, bali niihubiri Habari Njema; wala si kwa hekima ya maneno, msalaba wa Kristo usije ukabatilika.
Kristo aliye Nguvu na hekima ya Mungu
18 # 2 Kor 4:3; Rum 1:16 Kwa sababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu. 19#Isa 29:14 Kwa kuwa imeandikwa,
Nitaiharibu hekima yao wenye hekima,
Na akili zao wenye akili nitazikataa.
20 # Ayu 12:17; Isa 19:12; 33:18; 44:25 Yuko wapi mwenye hekima? Yuko wapi mwandishi? Yuko wapi mleta hoja wa nyakati hizi? Je! Mungu hakuifanya hekima ya dunia kuwa ni upumbavu? 21#Mt 11:25; Lk 8:12 Kwa maana katika hekima ya Mungu, dunia isipopata kumjua Mungu kwa hekima yake, Mungu alipenda kuwaokoa waaminio kwa upuzi wa lile neno linalohubiriwa. 22#Mt 12:38; Yn 4:48; Mdo 17:18,32 Kwa sababu Wayahudi wanataka ishara, na Wagiriki wanatafuta hekima; 23#1 Kor 2:14; Rum 9:32 bali sisi tunamhubiri Kristo, aliyesulubiwa; kwa Wayahudi ni kikwazo, na kwa Wagiriki ni upuzi; 24#Kol 2:3 bali kwao waitwao, Wayahudi kwa Wagiriki, ni Kristo, nguvu ya Mungu, na hekima ya Mungu. 25#2 Kor 13:4 Kwa sababu upumbavu wa Mungu una hekima zaidi ya wanadamu, na udhaifu wa Mungu una nguvu zaidi ya wanadamu.
26 # Mt 11:25; Yn 7:48; Yak 2:1-5 Maana, ndugu zangu, angalieni mwito wenu, ya kwamba si wengi wenye hekima ya mwilini, si wengi wenye nguvu, si wengi wenye cheo walioitwa; 27bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu; 28tena Mungu alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko; 29#Rum 3:27; Efe 2:9 mwenye mwili awaye yote asije akajisifu mbele za Mungu. 30#Yer 23:5,6; 2 Kor 5:21; Yn 17:19 Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyefanywa kwetu hekima itokayo kwa Mungu, na haki, na utakatifu, na ukombozi; 31#Yer 9:23,24 kusudi, kama ilivyoandikwa, Yeye aonaye fahari na aone fahari juu ya Bwana.

Currently Selected:

1 Wakorintho 1: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in