1 Petro 2
2
Jiwe hai na watu walioteuliwa
1 #
Efe 4:22; Yak 1:21 Basi, wekeni mbali uovu wote na hila yote, na unafiki na husuda na masingizio yote. 2#1 Kor 3:2; Ebr 5:12,13; Mt 18:3 Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu; 3#Zab 34:8 ikiwa mmeonja ya kwamba Bwana ni mwenye fadhili. 4#Zab 118:22; Isa 28:16; Mt 21:42; Mdo 4:11 Mmwendee yeye, jiwe lililo hai, lililokataliwa na wanadamu, bali kwa Mungu ni teule, lenye heshima. 5#Efe 2:21,22; Rum 12:1 Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa muwe nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo. 6#Isa 28:16; Rum 9:33 Kwa kuwa imeandikwa katika Maandiko:
Tazama, naweka katika Sayuni jiwe kuu la pembeni, teule, lenye heshima,
Na kila amwaminiye hatatahayarika.
7 #
Zab 118:22; Mt 21:42 Basi, heshima hii ni kwenu ninyi mnaoamini. Bali kwao wasioamini,
Jiwe walilolikataa waashi,
Limekuwa jiwe kuu la pembeni.
8 #
Isa 8:14-15; Rum 9:33 Tena,
Jiwe la kujikwaza mguu, na mwamba wa kuangusha.
Kwa maana hujikwaza kwa neno lile, wasiliamini, nao waliwekwa kusudi wapate hayo. 9#Kut 19:5-6; Isa 43:20-21; Kum 4:20; 7:6; 14:2; Tit 2:14; Isa 9:2; Mdo 26:18; 2 Kor 4:6; Efe 5:8; Flp 2:15; Ufu 1:6 Bali ninyi ni uzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu; 10#Hos 1:6,9; 2:1,23; Rum 9:25 ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa ni taifa la Mungu; mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata rehema.
Ishini kama watumishi wa Mungu
11 #
Zab 39:12; Gal 5:17,24; Efe 2:19; Yak 4:1 Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho. 12#Isa 10:3; Mt 5:16; Yak 3:13 Muwe na mwenendo mzuri kati ya Mataifa, ili, iwapo huwasingizia kuwa watenda mabaya, wayatazamapo matendo yenu mazuri, wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa.
13 #
Rum 13:1-7; Tit 3:1 Tiini kila kiamriwacho na watu, kwa ajili ya Bwana; iwe ni mfalme kama mwenye cheo kikubwa; 14au iwe ni watawala, kama wanaotumwa naye ili kuwalipiza kisasi watenda mabaya na kuwasifu watenda mema. 15#1 Pet 3:16 Kwa sababu ndiyo mapenzi ya Mungu, kwamba kwa kutenda mema mzibe vinywa vya ujinga vya watu wapumbavu; 16#Gal 5:13 kama walio huru, ila wasioutumia uhuru huo kwa kusitiri ubaya, bali kama watumwa wa Mungu. 17#Rum 12:10; Mit 24:21; Mt 22:21 Waheshimuni watu wote. Wapendeni ndugu. Mcheni Mungu. Mpeni heshima mfalme.
Mfano wa kuteswa kwa Yesu
18 #
Efe 6:5; Tit 2:9 Enyi watumishi, watiini bwana zenu kwa hofu nyingi, sio wale walio wema na wenye upole tu, bali pia wale walio wakali. 19Maana huu ndio wema hasa, mtu akivumilia huzuni kwa kumkumbuka Mungu, pale ateswapo pasipo haki. 20#1 Pet 3:14,17; 4:13,14; Mt 5:10 Kwa maana ni sifa gani kustahimili, mtendapo dhambi na kupigwa makofi? Lakini kustahimili, mtendapo mema na kupata mateso, huu ndio wema hasa mbele za Mungu. 21#Mt 16:24; Yn 13:15 Kwa sababu ndio mlioitiwa; maana Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, akawaachia kielelezo, mfuate nyayo zake. 22#Isa 53:9; Yn 8:46; 2 Kor 5:21 Yeye hakutenda dhambi, wala udanganyifu haukuwapo kinywani mwake. 23#Isa 53:7 Yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano; alipoteswa, hakutisha; bali alijikabidhi kwake yeye ahukumuye kwa haki. 24#Isa 53:5,12; 1 Yoh 3:5; Rum 6:11; Ebr 9:28 Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa. 25#Isa 53:6; Eze 34:5; 1 Pet 5:4; Yn 10:12 Kwa maana mlikuwa mnapotea kama kondoo; lakini sasa mmemrudia Mchungaji na Mwangalizi wa roho zenu.
Currently Selected:
1 Petro 2: SRUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.