1 Petro 4
4
Mawakili wema na neema ya Mungu
1 #
Rum 6:2,7 Basi kwa kuwa Kristo aliteswa katika mwili wake, ninyi nanyi jivikeni silaha ya nia ile ile; kwa maana yeye aliyeteswa katika mwili ameachana na dhambi. 2#1 Yoh 2:16,17 Tangu sasa msiendelee kuishi katika tamaa za wanadamu, bali katika mapenzi ya Mungu, wakati wenu uliobaki wa kukaa hapa duniani. 3#Efe 2:2,3; Tit 3:3 Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya Mataifa; kuishi katika uzinzi, tamaa, ulevi, na karamu za kula na kunywa vileo kupindukia, na ibada haramu ya sanamu; 4mambo ambayo wao huona kuwa ni ajabu ya ninyi kutokwenda mbio pamoja nao katika ufisadi ule ule usio na kiasi, wakiwatukana. 5#Mdo 10:42; 2 Tim 4:1; Rum 14:9,10 Nao watatoa hesabu kwake yeye aliye tayari kuwahukumu walio hai na waliokufa. 6#1 Pet 3:19; Rum 8:10; 1 Kor 5:5 Maana kwa ajili hiyo hata hao waliokufa walihubiriwa Injili, ili kwamba wahukumiwe katika mwili kama wahukumiwavyo wanadamu; bali wawe hai katika roho kama Mungu alivyo hai.
7 #
1 Kor 10:11; 1 Yoh 2:18 Lakini mwisho wa mambo yote umekaribia; basi, iweni na akili, mkeshe katika sala. 8#Mit 10:12; 1 Pet 1:22; Yak 5:20; 1 Kor 13:7 Zaidi ya yote iweni na bidii kubwa katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi. 9#Ebr 13:2 Mkaribishane ninyi kwa ninyi, pasipo kunung'unika; 10#Lk 12:42 kila mmoja kwa kadiri alivyoipokea karama, itumieni kwa kuhudumiana; kama mawakili wema wa neema mbalimbali za Mungu. 11#Rum 3:2; 12:7; 1 Kor 10:31 Mtu akisema, na aseme kama asemaye maneno halisi ya Mungu; mtu akihudumu, na ahudumu kwa nguvu anazojaliwa na Mungu; ili Mungu atukuzwe katika mambo yote kwa Yesu Kristo. Utukufu na uweza una yeye hata milele na milele. Amina.
Kuteseka kama Mkristo
12 #
1 Pet 1:6,7 Wapenzi, msione kuwa ni ajabu ule msiba ulio kati yenu, unaowapata kama moto ili kuwajaribu, kana kwamba ni kitu kigeni kiwapatacho. 13#Mdo 5:41; Yak 1:2; Rum 8:17; 2 Tim 2:12 Lakini kama mnavyoyashiriki mateso ya Kristo, furahini; ili pia katika ufunuo wa utukufu wake mfurahi kwa shangwe. 14#1 Pet 2:20; Isa 11:2; Zab 89:50,51 Mkilaumiwa kwa ajili ya jina la Kristo ni heri yenu; kwa kuwa Roho wa utukufu na wa Mungu anawakalia. 15Lakini pasiwe na hata mmoja wenu atakayeteseka kwa kuwa mwuaji, mwizi, mhalifu au hata mfitini. 16#Mdo 11:26; Flp 1:20 Lakini ikiwa mtu yeyote miongoni mwenu anateseka kwa sababu ni Mkristo, asione haya, bali amtukuze Mungu maana ana jina hili. 17#Eze 9:6; Yer 25:29; 2 The 1:8 Kwa maana wakati umefika wa hukumu kuanza katika nyumba ya Mungu; na ikianza kwetu sisi, mwisho wao wasioitii Injili ya Mungu utakuwaje? 18#Mit 11:31; Lk 23:31 Na mwenye haki akiokoka kwa shida, yule asiyemcha Mungu na mwenye dhambi ataonekana wapi? 19#Zab 31:5 Basi wao wateswao kwa mapenzi ya Mungu na wamwekee amana roho zao, katika kutenda mema, kama kwa Muumba mwaminifu.
Currently Selected:
1 Petro 4: SRUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.