YouVersion Logo
Search Icon

2 Mambo ya Nyakati 23

23
1 # 2 Fal 11:4 Katika mwaka wa saba Yehoyada alijasiri, akawatwaa makamanda wa mamia, Azaria mwana wa Yerohamu, na Ishmaeli mwana wa Yehohanani, na Azaria mwana wa Obedi, na Maaseya mwana wa Adaya, na Elishafati mwana wa Zikri, akapatana nao. 2#Zab 112:5 Wakazunguka katikati ya Yuda, wakawakusanya Walawi kutoka katika miji yote ya Yuda, na wakuu wa nyumba za mababa wa Israeli, wakaja Yerusalemu. 3#2 Sam 7:12; 1 Fal 2:4; 9:5; 2 Nya 6:16; 7:18; 21:7; Zab 89:29,36 Na kusanyiko lote wakafanya agano na mfalme nyumbani mwa Mungu. Akawaambia, Angalieni, mwana wa mfalme atatawala, kama BWANA alivyonena juu ya wana wa Daudi. 4#1 Nya 9:25; Lk 1:8,9 Hili ndilo neno mtakalolifanya; theluthi moja yenu, ninyi makuhani na Walawi mwingiao zamu siku ya sabato, mtalinda milangoni; 5#Mdo 3:2 na theluthi nyumbani pa mfalme; na theluthi langoni pa msingi; na watu wote watakuwapo nyuani mwa nyumba ya BWANA. 6#2 Fal 11:6,7; 1 Nya 23:28,29; Hes 16:5; Ezr 8:28 Wala asiingie mtu nyumbani mwa BWANA, ila makuhani, na Walawi watumikao; hao wataingia, kwa kuwa ni watakatifu; ila watu wengine wote watafuata amri za BWANA. 7Nao Walawi watamzunguka mfalme pande zote, kila mtu mwenye silaha zake mkononi; naye awaye yote aingiaye nyumbani na auawe; nanyi mfuatane na mfalme, aingiapo na atokapo.
Yoashi atawazwa kuwa Mfalme
8 # 1 Nya 24:1; 25:1 Basi Walawi na Yuda wote wakafanya kama alivyowaamuru Yehoyada kuhani; wakawatwaa kila mtu watu wake, hao watakaoingia siku ya sabato, na wale watakaotoka siku ya sabato; kwa maana Yehoyada kuhani hakuwaruhusu waondoke.
9Naye Yehoyada kuhani akawapa makamanda wa mamia mikuki, na ngao, na vigao, vilivyokuwa vya mfalme Daudi, vilivyokuwamo nyumbani mwa Mungu. 10Akawasimamisha watu wote, kila mtu akiwa na silaha yake mkononi, toka pembe ya kulia ya nyumba mpaka pembe ya kushoto, upande wa madhabahu na nyumba, kumzunguka mfalme pande zote. 11#Kut 25:16; 31:18; Kum 17:18; Zab 2:10,12; 78:5; Isa 8:16,20; 1 Sam 10:24; 2 Sam 16:16; 1 Fal 1:39 Ndipo wakamleta nje mwana wa mfalme, wakamvika taji, na kumpa ule ushuhuda,#23:11 Tazama Kut 25:16. wakamtawaza kuwa mfalme; Yehoyada na wanawe wakamtia mafuta, wakasema, Mfalme na aishi.
Athalia auawa
12Na Athalia alipoisikia sauti ya watu, na ya walinzi, na ya hao waliomsifu mfalme, akaingia kwa watu nyumbani mwa BWANA; 13#1 Nya 25:8; 1 Fal 18:17,18; Rum 2:3 akatazama, na angalia, mfalme amesimama karibu na nguzo yake mlangoni, nao makamanda na wenye parapanda karibu na mfalme; wakafurahi watu wote wa nchi, wakapiga parapanda; waimbaji pia wakipiga vinanda, wakaongoza nyimbo za kusifu. Ndipo Athalia akararua mavazi yake, akasema, Uhaini! Uhaini! 14#Hes 5:2; 19:14 Yehoyada kuhani akawaleta nje makamanda wa mamia, waliowekwa kuongoza jeshi, akawaambia, Mtoeni nje kati ya safu; na yeyote amfuataye, na auawe kwa upanga; kwani kuhani amesema, Msimwue katika nyumba ya BWANA. 15#Neh 3:28; Mwa 9:5; 2 Nya 22:10; Mt 7:2 Basi wakampisha njia; akaenda kwa kuingia pa mlango wa farasi nyumbani mwa mfalme; nao wakamwua huko.
16 # Kum 5:2,3; 2 Fal 11:17; 2 Nya 15:12; 29:10; Ezr 10:3; Neh 9:38 Kisha, Yehoyada akafanya agano, yeye na watu wote, na mfalme, kwamba watakuwa watu wa BWANA. 17#2 Fal 10:23; 11:18; 18:4; 2 Nya 34:4-7; Kum 13:9 Na watu wote wakaiendea nyumba ya Baali, wakaibomoa; wakavunjavunja madhabahu zake na sanamu zake, wakamwua Matani kuhani wa Baali mbele ya madhabahu. 18#1 Nya 23:6,30,31; 24:1; 25:2,6; Kut 29:38; Hes 28:2 Yehoyada akauamuru usimamizi wa nyumba ya BWANA chini ya mkono wa makuhani Walawi, aliowagawa Daudi nyumbani mwa BWANA, ili wazisongeze sadaka za kuteketezwa za BWANA, kama ilivyoandikwa katika Torati ya Musa, kwa kufurahi na kuimba, kama alivyoamuru Daudi. 19#1 Nya 26:1 Akawaweka walinzi malangoni pa nyumba ya BWANA, asiingie aliye najisi kwa namna yoyote. 20#2 Fal 11:19 Akawatwaa makamanda wa mamia, na watu wakubwa, na hao watawalao watu, na watu wote wa nchi, akamteremsha mfalme kutoka nyumba ya BWANA; wakalipitia lango la juu waende nyumbani kwa mfalme, wakamketisha mfalme katika kiti cha ufalme. 21#1 Sam 11:15; 1 Fal 1:40; 2 Fal 11:20; Zab 58:10; Mit 11:10; 29:2 Basi wakafurahi watu wote wa nchi, na mji ukatulia baada ya Athalia kuuawa kwa upanga.

Currently Selected:

2 Mambo ya Nyakati 23: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

Video for 2 Mambo ya Nyakati 23