YouVersion Logo
Search Icon

2 Mambo ya Nyakati 26

26
Utawala wa Uzia
1 # 2 Fal 14:21,22; 15:1 Na watu wote wa Yuda wakamtwaa Uzia, naye alikuwa mwenye miaka kumi na sita, wakamfanya awe mfalme mahali pa Amazia babaye. 2Huyo akajenga Elathi, akaurudisha kwa Yuda, baada ya kulala mfalme pamoja na babaze. 3Uzia alikuwa na umri wa miaka kumi na sita alipoanza kutawala; akatawala huko Yerusalemu miaka hamsini na miwili; na jina la mamaye aliitwa Yekolia wa Yerusalemu. 4Akafanya yaliyo ya adili machoni pa BWANA, sawasawa na yote aliyoyafanya Amazia babaye. 5#2 Nya 24:2; Mwa 41:15; Dan 1:17; 2:19; 10:1 Akajitia nia amtafute Mungu katika siku za Zekaria, aliyekuwa na fahamu katika maono ya Mungu; na muda alipomtafuta BWANA, Mungu alimfanikisha. 6#2 Nya 21:16; Isa 14:29 Akatoka akapigana na Wafilisti, akauvunja ukuta wa Gathi, na ukuta wa Yabne, na ukuta wa Ashdodi; akajenga miji katika Ashdodi na katikati ya Wafilisti. 7#1 Nya 5:20; 2 Nya 14:11; 21:16; Mdo 26:22 Mungu akamsaidia juu ya Wafilisti, na juu ya Waarabu waliokaa Gur-baali, na juu ya Wameuni. 8#Mwa 19:38; 1 Sam 11:1; 2 Sam 8:2; 2 Nya 17:11 Na Waamoni wakampa Uzia zawadi; likaenea jina lake mpaka Misri; alipata nguvu nyingi. 9#2 Fal 14:13; Neh 3:13,19,32; Zek 14:10 Tena Uzia akaujengea Yerusalemu minara, penye Lango la Pembeni, na penye Lango la Bondeni, na ugeukapo ukuta, akaitia nguvu. 10#2 Nya 21:16 Akajenga minara tena nyikani, akachimba mabwawa mengi, maana alikuwa na ng'ombe tele; katika Shefela pia, na katika nchi tambarare; tena alikuwa na wakulima na watunza mizabibu milimani, na katika mashamba ya neema; maana yeye alipenda ukulima.
11Zaidi ya hayo Uzia alikuwa na jeshi la watu wa kupigana, waliokwenda vitani vikosi vikosi, kulingana na hesabu walivyohesabu na Yeieli mwandishi, na Maaseya msimamizi, chini ya mkono wa Hanania, mmojawapo wa makamanda wa mfalme. 12Hesabu yote ya wakuu wa nyumba za mababa, watu mashujaa, ilikuwa elfu mbili na mia sita. 13Na chini ya mkono wao kulikuwa na jeshi la askari, elfu mia tatu na saba, na mia tano, ambao walipigana vita kwa nguvu nyingi, kumsaidia mfalme juu ya adui. 14Uzia akawapatia jeshi lote ngao na mikuki, na chapeo, na deraya za madini, na nyuta, na mawe ya kupiga kwa teo. 15Huko Yerusalemu akatengeneza mitambo ya vita, iliyobuniwa na watu mastadi, iwekwe juu ya minara na juu ya buruji, ili kurusha mishale na mawe makubwa. Jina lake likaenea mbali sana; kwa kuwa alisaidiwa mno ajabu, hata akapata nguvu.
Kiburi na ukaidi
16 # Kum 32:15; 2 Nya 25:19; 32:25; Hab 2:4; Kol 2:18; Kum 8:14; 2 Fal 16:12,13 Lakini alipokuwa na nguvu, moyo wake ulitukuka, hata akafanya maovu, akamwasi BWANA, Mungu wake; kwani aliingia hekaluni mwa BWANA, ili afukize uvumba juu ya madhabahu ya kufukizia. 17#1 Nya 6:10 Azaria kuhani akaingia nyuma yake, na pamoja naye makuhani themanini wa BWANA, mashujaa; 18#2 Nya 19:2; Yer 13:18; Mt 14:4; Gal 2:11; Hes 16:40; 18:7; Kut 30:7 wakamzuia Uzia mfalme, wakamwambia, Si haki yako, Uzia, kumfukizia BWANA uvumba, ila ni haki ya makuhani wana wa Haruni, waliofanywa wakfu, ili wafukize uvumba; toka katika patakatifu; kwa kuwa umekosa; wala haitakuwa kwa heshima yako kutoka kwa BWANA, Mungu. 19#Hes 12:10; 2 Fal 5:27 Uzia akakasirika; naye alikuwa na chetezo mkononi cha kufukizia uvumba; naye hapo alipowakasirikia makuhani, ukoma ukamtokea katika paji la uso wake mbele ya makuhani nyumbani mwa BWANA karibu na madhabahu ya kufukizia. 20#Est 6:12 Azaria kuhani mkuu na makuhani wote wakamtazama, na angalia, alikuwa na ukoma pajini mwa uso, wakamtoa humo upesi; hata na yeye mwenyewe akafanya haraka kutoka, kwa sababu BWANA amempiga. 21#2 Fal 15:5; Law 13:46; Hes 5:2 Uzia mfalme akawa na ukoma hadi siku ya kufa kwake, akakaa katika nyumba ya pekee, kwa kuwa ni mwenye ukoma; maana alitengwa na nyumba ya BWANA; na Yothamu mwanawe alikuwa kiongozi wa nyumba ya mfalme, akiwatawala watu wa nchi. 22#Isa 1:1 Basi mambo yote ya Uzia yaliyosalia, ya kwanza na ya mwisho, aliyaandika Isaya nabii, mwana wa Amozi. 23#Isa 6:1 Basi Uzia akalala na babaze; wakamzika karibu na babaze katika eneo la kuzikia la wafalme; kwa kuwa walisema, Huyu ni mwenye ukoma. Na Yothamu mwanawe akatawala mahali pake.

Currently Selected:

2 Mambo ya Nyakati 26: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

Video for 2 Mambo ya Nyakati 26