YouVersion Logo
Search Icon

2 Wakorintho 13

13
Maonyo zaidi
1 # Kum 17:6; 19:15; Mt 18:16; 1 Tim 5:19 Hii ndiyo mara yangu ya tatu kuja kwenu. Kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno litathibitishwa. 2Nimetangulia kuwaambia; na, kama vile nilipokuwapo mara ya pili, vivyo hivyo sasa nisipokuwapo, nawaambia wazi wao waliotenda dhambi tangu hapo, na wengine wote, ya kwamba, nikija, sitahurumia; 3kwa kuwa mnatafuta dalili ya Kristo, asemaye ndani yangu, ambaye si dhaifu kwenu, bali ana uweza ndani yenu. 4#Flp 2:7,8 Maana, alisulubiwa katika udhaifu, lakini anaishi kwa nguvu za Mungu. Maana sisi nasi tu dhaifu katika yeye; lakini tutaishi pamoja naye kwa uweza wa Mungu ulio kwenu. 5#1 Kor 11:28 Jichunguzeni wenyewe muone kama mmekuwa katika imani; jithibitisheni wenyewe. Au hamjijui wenyewe, kwamba Yesu Kristo yu ndani yenu? Isipokuwa iwe mmekataliwa. 6Lakini natumaini kama mtajua ya kuwa sisi hatukukataliwa. 7Nasi tunamwomba Mungu, msifanye lolote lililo baya; si kwamba sisi tuonekane tumekubaliwa, lakini ninyi mfanye lile lililo jema, ijapokuwa sisi tu kama waliokataliwa. 8#1 Kor 13:6 Maana hatuwezi kutenda neno lolote kinyume cha kweli, bali kwa ajili ya kweli. 9Maana twafurahi, iwapo sisi tu dhaifu, nanyi mmekuwa hodari. Tena twaomba hili nalo, kutimilika kwenu. 10#2 Kor 2:3; 10:8,11 Kwa sababu hiyo, naandika haya nikiwa mbali nanyi, ili, nikija, nisiwe na ukali wa kadiri ya uwezo ule niliopewa na Bwana, kwa kujenga wala si kwa kubomoa.
Salamu za mwisho na baraka
11 # Flp 4:4; Rum 15:33 Hatimaye, ndugu, kwaherini; mtimilike, mfarijike, nieni mamoja, mkae katika amani; na Mungu wa upendo na amani atakuwa pamoja nanyi. 12#1 Kor 16:20 Salimianeni kwa busu takatifu. Watakatifu wote wanawasalimu.
13Neema ya Bwana Yesu Kristo, na pendo la Mungu, na ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote.

Currently Selected:

2 Wakorintho 13: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in