YouVersion Logo
Search Icon

2 Wafalme 3

3
Yoramu atawala Israeli
1 # 2 Fal 1:17 Basi Yoramu#3:1 Au, Yehoramu. mwana wa Ahabu alianza kutawala juu ya Israeli huko Samaria katika mwaka wa kumi na nane wa Yehoshafati mfalme wa Yuda, akatawala miaka kumi na miwili. 2#1 Fal 16:31,32 Akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA; ila si kama baba yake na kama mama yake; maana akaiondoa ile nguzo ya Baali aliyoifanya baba yake. 3#2 Fal 10:28-31; 1 Fal 12:28-32 Pamoja na hayo alishikamana na dhambi za Yeroboamu mwana wa Nebati, ambazo kwa hizo aliwakosesha Israeli; wala hakuziacha.
Vita kati ya Israeli na Moabu
4 # Mwa 13:2; Ayu 1:3; Isa 16:1 Basi Mesha, mfalme wa Moabu, alikuwa mfuga kondoo; naye alikuwa akimlipa mfalme wa Israeli wana-kondoo elfu mia moja na sufu ya kondoo dume elfu mia moja. 5#2 Fal 1:1 Lakini ikawa, Ahabu alipokufa, mfalme wa Moabu akamwasi mfalme wa Israeli. 6Akatoka wakati ule ule mfalme Yoramu katika Samaria, akawahesabu Israeli wote. 7#1 Fal 22:4 Akaenda akatuma kwa Yehoshafati mfalme wa Yuda, akasema, Mfalme wa Moabu ameniasi; je! Utakwenda pamoja nami tupigane na Moabu? Akasema, Nitakwenda; mimi ni kama wewe, watu wangu ni kama watu wako, farasi wangu ni kama farasi wako. 8Akauliza, Njia ipi tuiendee? Akajibu, Njia ya jangwa la Edomu. 9#Kut 11:8 Basi mfalme wa Israeli akaenda, na mfalme wa Yuda, na mfalme wa Edomu; wakazunguka mwendo wa siku saba; wala hapakuwa na maji kwa jeshi, wala kwa wanyama waliowafuata. 10#Zab 78:34; Mit 19:3; Isa 8:21 Mfalme wa Israeli akasema, Ole wetu! Kwani BWANA amewakutanisha hawa wafalme watatu, awaue mkononi mwa Moabu.
11 # 1 Fal 22:7; Amo 3:7; 1 Nya 22:12; Zab 55:22; Mit 3:5,6 Lakini Yehoshafati akasema, Je! Hakuna nabii yeyote hapa wa BWANA ili tumwulize yeye shauri la BWANA? Akajibu mtumishi mmoja wa mfalme wa Israeli, akasema, Yupo hapa Elisha mwana wa Shafati, aliyekuwa akimimina maji juu ya mikono yake Eliya. 12#2 Fal 2:25 Yehoshafati akasema, Neno la BWANA analo huyu. Basi mfalme wa Israeli, na Yehoshafati, na mfalme wa Edomu, wakamshukia. 13#Eze 14:3; Amu 10:14; Rut 1:15; 1 Fal 18:19 Elisha akamwambia mfalme wa Israeli, Nina nini mimi nawe? Uende kwa manabii wa babayo, na manabii wa mamayo. Mfalme wa Israeli akamwambia, La, sivyo; kwa kuwa BWANA amewakutanisha hawa wafalme watatu, awaue mkononi mwa Moabu. 14#1 Fal 17:1; 2 Fal 5:16; Zab 15:4 Elisha akasema, Kama BWANA wa majeshi aishivyo, ambaye nimesimama mbele zake, kama singemwangalia uso wake Yehoshafati mfalme wa Yuda, singekutazama, wala kuonana nawe. 15#1 Sam 10:5; Eze 1:3; 3:14,22; 8:1 Ila sasa niletee mpiga kinanda. Ikawa, mpiga kinanda alipokipiga, mkono wa BWANA ukamjia juu yake. 16#2 Fal 4:3 Akasema, BWANA asema hivi, Fanyeni bonde hili lijae mahandaki. 17#Zab 107:35 Kwa kuwa BWANA asema hivi, Hamutauona upepo, wala hamtaiona mvua, ila bonde hilo litajaa maji; nanyi mtakunywa, ninyi, na ng'ombe zenu, na wanyama wenu. 18#Yer 32:17,27; Mk 10:27; Lk 1:37; Efe 3:20; 1 Fal 20:28 Na jambo hili ni jepesi machoni pa BWANA; pia atawatia Wamoabi mikononi mwenu. 19#1 Sam 15:3 Nanyi mtapiga kila mji wenye boma, na kila mji ulio mzuri, na kila mti mwema mtaukata, na chemchemi zote za maji mtaziziba, na kila mahali palipo pema mtapaharibu kwa mawe. 20#Kut 29:39,40 Ikawa asubuhi, wakati wa kutoa sadaka ya unga, tazama, maji yakaja kwa njia ya Edomu, hata nchi ikajaa maji.
21Basi Wamoabi wote waliposikia ya kuwa wafalme hao wamekwea ili kupigana nao, walijikusanya pamoja, wote wawezao kuvaa silaha, na wenye umri zaidi, wakasimama mpakani. 22Wakaamka asubuhi na mapema, na hilo jua likametameta juu ya maji, na Wamoabi wakayaona yale maji yaliyowaelekea kuwa ni mekundu kama damu. 23Wakasema, Ndiyo damu hii; bila shaka hao wafalme wameharibika, wamepigana wenyewe kwa wenyewe; basi sasa, enyi Wamoabi, nyara hizo! 24Hata walipokuja kambini mwa Israeli, Waisraeli wakainuka wakawapiga Wamoabi, hata wakakimbia mbele yao; wakaendelea wakiwapiga Wamoabi hadi kwao. 25#Isa 16:7,11 Wakaibomoa ile miji; wakatupa katika kila mahali palipo pema kila mtu jiwe lake, wakapajaza; wakaziziba chemchemi zote za maji, wakaikata miti yote iliyo mizuri; mpaka katika Kir-haresethi tu wakayasaza mawe yake; ila wenye kombeo wakauzunguka wakaupiga. 26Naye mfalme wa Moabu alipoona ya kwamba ameshindwa vitani, alitwaa pamoja naye watu mia saba wenye kufuta panga ili wapenye hata kwa mfalme wa Edomu; wala hawakudiriki. 27#Amo 2:1; Law 18:21; 20:2; Kum 12:31; 18:10; 2 Fal 17:17; 2 Nya 28:3; Zab 106:37,38; Yer 7:31; 32:35; Eze 16:20; 23:37 Ndipo akamtwaa mwanawe wa kwanza, yeye ambaye angetawala mahali pake, akamtoa awe sadaka ya kuteketezwa juu ya ukuta. Kukawa hasira kuu juu ya Israeli; basi wakatoka kwake, wakarudi kwenda nchi yao wenyewe.

Currently Selected:

2 Wafalme 3: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

Video for 2 Wafalme 3