2 Timotheo 2
2
Askari mwema wa Yesu Kristo
1Basi wewe, mwanangu, uwe hodari katika neema iliyo katika Kristo Yesu. 2Na mambo yale uliyoyasikia kwangu mbele ya mashahidi wengi, hayo uwakabidhi watu waaminifu watakaofaa kuwafundisha wengine vile vile. 3#2 Tim 1:8; 4:5 Ushiriki taabu pamoja nami, kama askari mwema wa Kristo Yesu. 4Askari aliye vitani hajiingizi katika shughuli za dunia, maana lengo lake ni kumpendeza yeye aliyemweka kuwa askari. 5#2 Tim 4:8 Hata mwanariadha hapewi taji, asiposhindana kwa kufuata sheria. 6#1 Kor 9:7,10 Yampasa mkulima mwenye bidii ya kazi kuwa wa kwanza wa kupata fungu la mavuno. 7Yatafakari sana hayo nisemayo, kwa maana Bwana atakupa ufahamu katika mambo yote. 8#Rum 1:3; 2:16; 1 Kor 15:4,20; 2 Sam 7:12 Mkumbuke Yesu Kristo, aliyefufuka katika wafu, wa uzao wa Daudi kama inenavyo Injili yangu. 9#Efe 3:1,13; Flp 1:12-14; 2:17 Nami katika hiyo nimeteswa hata kufungwa kama mtenda mabaya; lakini neno la Mungu halifungwi. 10#Kol 1:24 Kwa ajili ya hilo nastahimili mambo yote, kwa ajili ya wateule, ili wao nao waupate wokovu ule ulio katika Kristo Yesu, pamoja na utukufu wa milele.
11 #
2 Kor 4:11
Ni neno la kuaminiwa. Kwa maana,
Kama tukifa pamoja naye,
tutaishi pamoja naye pia;
12 #
Mt 10:33; Lk 12:9 Kama tukistahimili,
tutamiliki pamoja naye;
Kama tukimkana yeye,
yeye naye atatukana sisi;
13 #
Rum 3:2,3; Hes 23:19 Kama sisi hatuamini,
yeye hudumu wa kuaminiwa.
Kwa maana hawezi kujikana mwenyewe.
Mtendakazi anayekubaliwa na Mungu
14 #
1 Tim 6:4; Tit 3:9 Uwakumbushe mambo hayo, ukiwaonya machoni pa Mungu, wasiwe na mashindano ya maneno, ambayo hayana faida, bali huwaharibu wanaoyasikia. 15#1 Tim 4:6; Lk 12:42; Tit 2:7,8 Jitahidi kujionesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mfanyakazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli. 16#1 Tim 4:7 Jiepushe na maneno machafu yasiyo na maana, ambayo si ya dini; kwa kuwa wataendelea zaidi katika maovu, 17#1 Tim 1:20 na neno lao litaenea kama donda ndugu. Miongoni mwa hao wamo Himenayo na Fileto, 18waliopotoka kutoka kwenye kweli, wakisema ya kwamba kiyama imekwisha tokea, hata kuipindua imani ya watu kadhaa. 19#Hes 16:5,26; Yn 10:14; Isa 26:13; 28:16,17 Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama, wenye mhuri huu,
Bwana awajua walio wake.
Na tena,
Kila aliitaye jina la Bwana na auache uovu.
20 #
1 Kor 3:12
Basi katika nyumba kubwa havimo vyombo vya dhahabu na fedha tu, bali na vya mti, na vya udongo; vingine vina heshima, vingine havina. 21#2 Tim 3:17 Basi ikiwa mtu amejitakasa kwa kujitenga na hao, atakuwa chombo cha kupata heshima, kilichosafishwa, kimfaacho Bwana, kimetengenezwa kwa kila kazi iliyo njema. 22#1 Tim 6:11; 1:5 Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi. 23#1 Tim 4:7 Lakini uyakatae maswali ya upumbavu yasiyo na elimu, ukijua ya kuwa huzaa magomvi. 24#Tit 1:7 Tena haimpasi mtumwa wa Bwana kuwa mgomvi; bali kuwa mwanana kwa watu wote, awezaye kufundisha, mvumilivu; 25#1 Tim 2:4 akiwaonya kwa upole wao washindanao naye, ili kama ikiwezekana, Mungu awajalie ili watubu na kuijua kweli; 26wapate tena fahamu zao, na kutoka katika mtego wa Ibilisi, ambaye amewanasa, hata wakayafanya mapenzi yake.
Currently Selected:
2 Timotheo 2: SRUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.